Redio One: Tumshaurini msichana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Redio One: Tumshaurini msichana!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ngekewa, May 31, 2012.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hii imetoka Redio One: NI hivi: Msichana mrembo ambae alikuwa akifuatwa na wanaume wengi aliamuwa kukubali kuanguka kwa kijana alieonekana amenona. Mapenzi yakanawiri na Kijana akitowa vyake ikiwa pamoja na Gari la Kifahari. Bahati mbaya kijana kashitakiwa kwa wizi kwenye kampuni yake na akawekwa ndani na hali haionyeshi kuwa atatoka karibuni.
  Msichana kwa kuthamini penzi lake na la mwenziwe akaamuwa kumuhakikishia kuwa yuko pamojanae ndani ya shida. Akakubali kuvaa pete ya uchumba iliyoshuhudiwa na marafiki wachache wakiwa kule detention. Msichana akawaakienda kule kizuizini huku akimpelekea mchumba wake mahitaji.
  Kilichotokea baadae ni kuwa msichana anapokwenda kizuizini anakutana na wazee wa yule kijana na wazee wanaonekana kumyanyapaa msichana.
  Anachofikiri msichana na hali hii nzima ni kuwa;
  1. Yeye ni mrembo na wengi walishamfuata sasa kwanini asumbuliwe, jee aachane nae atafute mwengine?
  2. Jee awambie wazee wa kijana kuwa wao ni wachumba? lakini hii itasaidia kitu iwapo uhusiano wenyew uko hivyo?
  Wana JF nini mtazamo wenu?
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ntarudi ngoja nimpigie ant sadaka anipatie desa!
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Yani wazo lake la kwanza ni kuwa "Yeye ni mrembo na wengi walishamfuata'!!!!

  Namshauri tu amwache huyo jamaa maana inaonekana huyo mdada hana mapenzi ya kweli, bali anajali urembo wake...

  Kama anadhani urembo mali, mwambie aende Jolly na Ambience, akawaulize wale warembo kule kwa nini wanajiuza... pambaf...
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye bold ndipo panapoleta matatizo. Mbona kijana hana kosa lolote? Kumuacha ni kuzidi kumtia unyonge kijana.
   
Loading...