Ujumbe Murua huu! Thanks Nazjaz.Why boasteth thyself, Oh, evil men; Playing smart, And not being clever?
I said, you're working iniquity, To achieve vanity (if a-so a-so); But the goodness of Jah, Jah
I-dureth for-I-ver, So if you are the big tree, We are the small axe. Ready to cut you down (well sharp), To cut you down
These are the words; Of my master, keep on tellin' me, No weak heart,Shall prosper ......
To cut you down
Sharpened ...
Kwa yale anayoyafanya Tendwa hivi sasa ni kama vile anauambia hivyo ulimwengu. Na kile kitendo cha kutangaza hadharani kwamba hawezi kuifuta CCM, bali anaweza kuvifuta vyama vingine, ni sawa na kuweka bayana kwamba maamuzi yake hayafanywi kwa misingi ya sheria za vyama vya siasa. Utendaji kazi wa huyu mzee kwa sasa ni highly questionable.ccm is above the law
Hata Red Brigade pia inaweza kufanya shughuli za ujasiliamali kama wafanyavyo Green Guard kwani shida iko wapi? Watu wamebaki kuweweseka na jina. Ni kweli bora CHADEMA wakiite kikundi chao Red Guard tuone kelel zitatoka wapi tena.
Nimeisoma mwenyewe kwa macho yangu hotuba ya Mbowe. Na sijaona popote anaposema kwamba hiki kikundi kitakuwa cha kijeshi. Zaidi sana amesema kiimarishwe kwa ajili ya ulinzi. Kwanini CCM mnakiogopa sana hiki kikundi? Mnadhani kitapata mafunzo kutoka wapi? Kwanini serikali isiwaache CHADEMA wakiboreshe, lakini wafuatilie kuona ni mambo gani ambayo hao vijana watafundishwa huko makambini?jina lolote lile, lazima hicho kikundi kitasambaratishwa na JWTZ. hii ni kutokana na malengo aliyoyataja mbowe juzi. ni kikundi hatari sana! leo mbowe kajamba pale central alipo banwa kuhusu red brigade. ccm na cuf vikundi vyao ni vya ulinzi wa kawaida. red brgd malengo yake ni vikundi vya kivita na mauaji. mbowe aswekwe ndani. tumechoka
Labda wapige marufuku pia salamu ya peopleeeees poweeeeeer, vinginevyo chadema itazaliwa upya kupitia mgombea binafsi na itachukua nchi. Chadema kama tufani, haikingwi kwa mwavuli.waache wafute ndio wtajua CCM inapendwa na nani
Ndugu zangu,
Hapa ndipo ninasema inawezekana tatizo ni jina. Maana CUF ambao wana blue guard hakuna anayewauliza. CCM wana green guard hakuna anayewauliza. Basi CHADEMA nao wabadilishe jina la kikundi chao na kukiita red guards. Labda kinachowasumbua hawa wakubwa ni jina hilo la red brigade.
Ndiyo maana kwenye hoja yangu ya msingi ninamshauri Tendwa aitishe mjadala na vyama vyote vya siasa ili waamue juu ya suala la ulinzi liweje. Lakini kuwapigia kelele wachache huku wengine wana vikundi kama hivyo, haikubaliki.mimi sijadili kama ccm. najadili kama mtanzania mwenye haki ya kuishi kwa amani. kila sehemu chdm wanapotia mguu ni vifo tu. kimeanza kuonekana kama chama cha kigaidi. kuna vikundi vya ulinzi visivyo tokana na vyama vya siasa hivyo vinaruhusiwa. vile vya vyama vya siasa vipigwe marufuku. Tanzania kwanza, siasa baadaye
suingi mkono chama cha siasa chochote kuwa na vikosi vikubwa vya ulinzi. hali hiyo itahatarisha amani. msajili avionye vyote vifute vikundi vyake. nia ilikua njema lkn hotuba ya mbowe na msisitizo aliyoutoa kuwa hawatohitaji tena ulinzi wa polisi ndiyo imetuamsha wananchi. chdm futeni red brgd. mtakumbana na mkono wa chuma wa JWTZ. ccm tuelezeni malengo ya green grds. mnasema ni vikosi vya ujasiriamali. kama malengo hayaeleweki na nyinyi futeni upuuzi wa green guards. cuf futeni blue guards. nchi ibaki salama ikilindwa na polisi pamoja na jwtzscramble; Embu tuambie malengo ya Green Guards na kazi zake ambazo jeshi la polisi, JWTZ na UWT hawawezi kufanya ili kuimarisha usalama. Katika majibu yako usilete umburula wa Green Guards kueneza sera za chama kwa sababu kazi hiyo inaweza kufanywa na Makatibu wenezi wa ngazi zote.Pia sera inawezekana kuenezwa na UVCCM,Jumuiya ya wazazi,umoja wa wanawake n.k Tuambie, mafunzo ya kurusha mateke,kujihami,ushushushu na kutumia siraha wanayopewa Green Guards ni kwa ajili ya nini?
Well, nimelijadili jambo hili kwa mapana kwa kuzingatia uwepo wa vikundi vingine vyenye majina mfanano ambavyo haviguswi. Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa karibu utakumbuka kwamba jina la red brigade limezua mjadala mkubwa sana hapa jamvini siku za hivi karibuni kupitia kwa Mwigulu Nchemba. Kwahiyo ni dhahiri kwamba hawa wenzetu wanatishwa zaidi na jina kuliko aina ya kazi ambazo kikundi hiki kitazifanya. Ndiyo maana nashawishika kwamba CHADEMA wabadili jina. Lakini kubadilika kwa majina pia si kitu kigeni, jina linabadilika kulingana na mazingira. Tulibadili jina la nchi kutoka Tanganyika hadi Tanzania tutashindwaje kubadili jina la kikundi tu?Ipo siku CCM watakutisha utabadili jina lako, na tena ipo siku utashauri CHADEMA ibadili jina.
Well, nimelijadili jambo hili kwa mapana kwa kuzingatia uwepo wa vikundi vingine vyenye majina mfanano ambavyo haviguswi. Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa karibu utakumbuka kwamba jina la red brigade limezua mjadala mkubwa sana hapa jamvini siku za hivi karibuni kupitia kwa Mwigulu Nchemba. Kwahiyo ni dhahiri kwamba hawa wenzetu wanatishwa zaidi na jina kuliko aina ya kazi ambazo kikundi hiki kitazifanya. Ndiyo maana nashawishika kwamba CHADEMA wabadili jina. Lakini kubadilika kwa majina pia si kitu kigeni, jina linabadilika kulingana na mazingira. Tulibadili jina la nchi kutoka Tanganyika hadi Tanzania tutashindwaje kubadili jina la kikundi tu?
Utakuwaumesoma headline wala hujasoma content yote...!Ipo siku CCM watakutisha utabadili jina lako, na tena ipo siku utashauri CHADEMA ibadili jina.