Real Madrid wamemchukia baniani lakini wanakipenda kiatu chake.

Real Madrid wamemchukia baniani lakini wanakipenda kiatu chake.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,711
Reaction score
1,738
Kwanza napenda kuwapa hongera kwa kutufunga 'El classico' ya jana ila mmethibitisha ule msemo wa "Baniani mbaya, kiatu chake kizuri". Staili mliyoitumia ni ile ile aliyokuwa akiitumia Jose Mourinho kila tukutanapo! Mbona mkikutana na timu nyingine hasa Atletico Madrid hampaki basi na kushambulia kwa kuvizia?
 
Bado hujaeleweka unataka kusema nini kwenye bandiko lako ndugu. Au ulikuwa unamaanisha Real Madrid wanamchukia Mourinho? Kama ndio hivyo wazo hilo ondoa. Jose Mourinho kaondoka Madrid bado anapendwa na anahitajika, na watu wengi walifikiri timu itateteleka bila yule mpotugizi lakini ni tofauti.

Jose Mourinho anapenda kufundisha soka Uingereza na alikuwa anathibisha hilo mara nyingi kwa kauli yake mwenye. Na kwa taarifa tu, Mourinho alinunua nyumba London miaka miwili nyuma kabla ya kwenda Chelsea.
Na siku yoyote Chelsea wakija Santiago Benarbeu, utaona mashabiki watatoa applause kwasababu kafanya mambo ya kupewa shukrani pale.

Style ya mchezo waliotumia Real Madrid jana ndio ilipangwa kwa ajili ya ushindi. Walitakiwa wacheze mpira kwa 100%, hakuna kutoa nafasi kwa wakatalani hata kiduchu. Goli alilofunga Neymar, ndio liliwaamsha kwamba kila kitu pale ni serious. Pepe na Marcelo wameongea leo kuwa wanacheza mpira kwa ajili ya wapenzi, na hiyo ndio soka ya Bernabeu.

Real Madrid huwezi kucompare na klabu nyingine tu, ile ni ROYAL. Not just a football club like you think about, it's a tribe. Kitu chochote lazima kifanyike kulinda heshima ya tribe, ndio maana inaitwa REAL.
 
Kama kungekuwa na hakimiliki kwenye mifumo ya mpira, mwenyehakimiliki ya kupaki basi asingekuwa Maximo. Tangu mpira ulipoanza kuchezwa, ilikuwani kawaida kurundika wachezaji wengi nyuma, ndio maana ukiangalia majina rasmi ya nafasi za uchezaji utakuta nyingi zinatamka waziwazi kwamba ni wachezaji wa kubaki nyuma: Goal keeper, full backs (2), half backs (2), centre half back. Yaani wachezaji hao sita walipaswa kupaki basi muda wote, la sivyo wangekuwa wamesaliti majukumu yao. Changamoto zilizofuatia ndiyo taratibu zikaondokana na hali hiyo, ambazo katika mageuzi ya kiuchezaji yanayotokana na mabadiliko ya sheria, kanuni, utaalamu na kwa hivyo uwezo wa wachezaji, hatimaye utaratibu huu wa kuwa na wachezaji nyingi nyuma ukarudiwa - lakini kwa kuongeza watu zaidi.
 
Back
Top Bottom