Beki huyo muhimu kwenye kikosi cha Los Blancos ataukosa mchezo wa Jumanne dhidi ya APOEL kufuatia jeraha la pua katika mechi dhidi ya Atletico
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya zinaendelea tena wiki hii klabu kadhaa zikiwa zimeshaweka hadharani vikosi vitakavyocheza, Real Madrid ikiwa miongoni mwao.
Lakini mlinzi Sergio Ramos ameachwa nje kikosi cha Real Madrid kitakachocheza dhidi ya APOEL kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuvunjika pua yake kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Atletico Madrid.
Kikosi cha Zinedine Zidane kimeundwa na wachezaji: Casilla, Moha, Carvajal, Vallejo, Varane, Nacho, Marcelo, Theo, Achraf, Kroos, Modric, Casemiro, Marcos Llorente, Asensio, Isco, Caballos, Ronaldo, Benzema, Lucas Vazquez, na Borja Mayoral.
Majeruhi wengine ukiachana na Ramos ambaye anatarajiwa kuwa nje ya kikosi hicho kwa siku kumi ni Keylor Navas na Gareth Bale huku habari njema ni juu ya urejeo wa Kovacic licha ya kutojumuishwa kwenye kikosi hicho.