@BAK hata mimi nimesoma leo, kwenye mitandao ndio habari yenyewe hiyo. Kama vipi bora Perez achukue hela tu kabla hajashuka bei, halafu ananunua vijana wenye uchungu wa maisha waje kupachika mabao. CR7 ashakuwa tajiri yule.
Machale yamemcheza anataka kurudisha ngawira zake before it is too late to do so. MANU wanaweza kumtaka tena maana bado ni kipenzi chao.
Lakini bei vilevile itategemea na perfomance yake kwenye hii miezi iliyobaki, summer ikifika anatakiwa awe anaongoza kwa mabao, lakini ikiwa na mwendo wa kusuasua sijui nani atalipa €200, sijui ndugu yake Morinho.
Ndio hapo utakaposhangaa Mkuu, timu mbali mbali kuanza kumgombea huyu. Ngoja tuangalie itakuwaje lakini mimi kwa maoni yangu jamaa bado ni mzuri sana kufikia hitimisho kwa ile mechi moja sikumtendea haki kabisa.