REA na ucheleweshaji usambazaji wa umeme

REA na ucheleweshaji usambazaji wa umeme

Dig the EA

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
287
Reaction score
279
Miezi kadhaa sasa kumekuwa na tatizo la kuchelewesha kusambaza Umeme. Kwa maana unakuta wanaweka nguzo, lkn kuja kuweka nyaya za umeme inaweza kuchukua miezi hata minne.

Haitatosha kuja kufunga na kuwasha generator yaweza kuchukua miezi mitatu na zaidi.

Pia kuja kuja kukagua, kutoa control number yaweza kuchukua miezi si Chini ya mitano. Wananchi wakipewa control number anaamini muda si mrefu ataunganishiwa umeme kwenye nyumba yake, lkn aweza kusubiri miezi mingine kadhaa hata zaidi ya mitatu minne.

Yaani kwa maneno mengine, zoezi la kuunganishwa umeme linachukua zaidi ya mwaka na nusu, karibia miaka miwili! Hii ni kutokuwa serious

Lkn mbaya zaidi siku za hivi karibuni kuna maeneo watu wakionyesha nia ya kutoa chochote, wanashughulikiwa haraka na kuwashiwa umeme.

Au mtu binafsi akitoa chochote anawashiwa umeme huku wengine mkirndelea kusubiri miezi na miezi.

Huduma hii ni kama siku za hivi karibuni inafanya makususudi kuchelewesha kusambaza Umeme ili watu watoe pesa.

Kuna harufu ya rushwa huko!
 
Toka corona imeanza upatikani wa material kutoka nje za nchi umekuwa wa taabu. Kwa vinavyopatikana ndani wapo ontime ndio kama hayo manguzo.
 
Basi sababu hizo wawaambie wananchi wajue, kimya kinakuwa kingi kiasi cha wananchi kutokujua kinachoendelea. Lkn mbona materials nyingi zinatengenezwa hapa nchini!?
wakandarasi walikuwa tayari wana stock kubwa tu ya material
 
Basi sababu hizo wawaambie wananchi wajue, kimya kinakuwa kingi kiasi cha wananchi kutokujua kinachoendelea. Lkn mbona materials nyingi zinatengenezwa hapa nchini!?
Kuna material wanachukua ndani na kuna material wanachukua nje, material ndani pia yamependa sana bei wengi wao wanaagiza nje. Viongozi wa ngazi za mikoa huwa wana majibu ila mahusiano ( mawasiliano ), ila pia wapo wakandarasi wazembe ambao ni tatizo la miradi kuchelewa
 
Nadhani hiyo sababu ya mwisho inaweza kuwa na mchango mkubwa, maana kuna maeneo/kanda ambapo shida hizi hazipo hivo.....
 
Huo ndo ukweli, watu hawataki kukubali lkn kipindi hiki Rea wanasuasua sana
Maneno kuwa Magufuli ni dikteta yalitawala sana kipindi cha uhai wake.

Namuomba Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.
 
Mtetezi wa wanyonge ameshaondoka sasa hivi hata ukisema kazi bure tu hakuna anaekusikiliza
Kanda ya ziwa hususani wilaya ya Kahama na halmashauri zake(halmashauri ya Msalala) na Maeneo kadhaa ya Buswelu, Ilemela jijini Mwanza
 
Hata wailaya ya Chato na geuta iko ovyo katika kuhudumiwa na REA na Tanesco
 
Back
Top Bottom