RC SIMIYU: Madini yametuingizia shilingi bilioni 135

John John Msakuzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
295
Reaction score
103


Akiongea na wanahabari, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Annamringi Macha amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2025 chini ya Rais Samia, Dhahabu zenye uzito wa gramu 1,301,842.81 zenye thamani ya shilingi bilioni 134.78 zimeuzwa kupitia soko la madini la Mkoa, ambapo shilingi bilioni 9.43 zimekusanywa kama mrahaba na ada za ukaguzi.

Aidha, amesema leseni za wachimbaji wadogo zimeongezeka kutoka 126 mwaka 2020 hadi 573 mwaka 2025, jambo linaloashiria ongezeko la shughuli za uchimbaji na ushiriki mpana wa wananchi katika sekta ya madini, ikiwemo vikundi vya wanawake waliopata leseni za uchimbaji.
​
 
Hayo madini yanachimbwa wapi hapo Simiyu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…