RC Mrisho Gambo: Marufuku maafisa TRA kuongozana na askari wenye mtutu kukusanya kodi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,067
10,936
RC Arusha, Mrisho Gambo amepiga marufuku maafisa wa TRA kuandamana na Polisi wenye silaha wanapokuwa kwenye shughuli za ukusanyaji kodi.

TRA.png
 
Wazo zuri ni TRA inatakiwa watoe Elimu kwa wanaolipa kodi ili wajue umuhimu wa kulipa kodi bila shurti na kuwa na makadirio yanayowiana na biashara watu wanataka kulipa kodi ndio maana kubadilisha TIN tuu unaona foleni wanakaa hata siku nzima kwa ishu hiyo wangekua hawataki wasingesubiri hizo TIN..
 
Amejua sababu ya Maafisa TRA kuambatana na jeshi la polisi wakati wa ukusanyaji kodi zao kwa Arusha....?Anyway kwa wafanyabiashara ni habari njema sana maana Maafisa TRA walikuwa wakivamia maduka wakiwa na hao maaskar kama wapo vitani...
 
Huyu anasema marufuku, kesho baba yake Bashite atasema waende na askari.
 
Amejua sababu ya Maafisa TRA kuambatana na jeshi la polisi wakati wa ukusanyaji kodi zao kwa Arusha....?Anyway kwa wafanyabiashara ni habari njema sana maana Maafisa TRA walikuwa wakivamia maduka wakiwa na hao maaskar kama wapo vitani...
Ila tatizo litakuja kwenye kuzilinda hizo pesa wanazozikusanya .............. imagine wamezunguka siku nzima na wamekusanya million 10. Hivi wahuni wakijua si watazifanyia mpango!!?

Haiwezekani ukawa unakusanya pesa ya serikali bila ulinzi. Ila kazi ya hao askari ndiyo inabidi iwe defined!!
 
Wazo zuri ni TRA inatakiwa watoe Elimu kwa wanaolipa kodi ili wajue umuhimu wa kulipa kodi bila shurti na kuwa na makadirio yanayowiana na biashara watu wanataka kulipa kodi ndio maana kubadilisha TIN tuu unaona foleni wanakaa hata siku nzima kwa ishu hiyo wangekua hawataki wasingesubiri hizo TIN..
Haya mawzo alishauriwa na baadhi ya rafiki zake wafanyabiashara wa mahoteli kuwa awashauri tra watoe elimu badala ya kukusanya kodi kwa kutumia nguvu ya jeshi
 
Hao maafisa wanataka waturudishe kwenye enzi za ukoloni nini?? Nchi hii ya Amani mtutu wa nini??
 
Umesema point kabisa
Gambo alikuwepo hotel flani pembeni ya cafe la azizi pale makao mapya siku ya alhamisi, mwenye hotel alimwambia adha wanazopata kwa tra kwa kutumia nguvu ya polisi na jeshi. Hii ni mbaya sana, watu wanahitaji elimu ili walipe kodi kwa hiari kwani kodi ni muhimu
 
Mkuu watu wanapata pressure kutoka juu hivyo wanafanya kazi kwa pressure zaidi kuliko kutumia elimu zao.
 
Ila tatizo litakuja kwenye kuzilinda hizo pesa wanazozikusanya .............. imagine wamezunguka siku nzima na wamekusanya million 10. Hivi wahuni wakijua si watazifanyia mpango!!?

Haiwezekani ukawa unakusanya pesa ya serikali bila ulinzi. Ila kazi ya hao askari ndiyo inabidi iwe defined!!
Nadhani ni busara kwanza mkuu wa mkoa angekaa na pande hizo mbili yaani TRA na jeshi la polis apate nikipi chanzo hasa cha kutumia vyombo vya ulinzi kwenye zoezi la kukusanya kodi ingawa sijajua kama kalifanya hilo , maana kama kafanya maamuzi bila kujadiliana na makundi haya naona kuna hatari mbele
 
Kutumia Polisi wakati wa kukusanya kodi, ni upungufu mkubwa kwa TRA.

Kuna taratibu za kisheria za kufuata katika ukusanyaji. Hilo la kuzunguka na mitutu ya bunduki halimo katika sheria. Hiyo inaashiria uonevu kwa walipa kodi. Wanataka kuwatisha ili waridhie hata pale ambapo huenda makadirio ya kodi siyo sahihi.
 
Back
Top Bottom