RC Mpya Morogoro akaribishwa na wizi wa mabox 40 ya dawa Ulanga

Yule RC wa kwanza kutumbuliwa Moro sijui Dr Rajab nanii atakuwa Wapi sijui maana kapotea kabisa
haaa haaa umenikumbusha nadhani DR.Rajabu Mtengwe kama sikosei yule alitumbuliwa mkoa wa Katavi akawa analialia rti aonewe huruma sijui kwa alizaliwa kuwa mkuu wa mkoa.Yule alibebwa na JK sijui kapotelea wapi daa siasa bwana.
 
Moro inaonekana ni pagumu kiaina. Wapelekewe RC Gen. wa Jeshi.
Mkoa huu ulishawahi kupata mkuu wa mkoa afisa wa jeshi mstasfu, Brig General Kalembo, lakini hakuweza kuunyosha kisawasawa. Vilevile ulishawahi kupata RC kocha was mpira hsyati Bendera lakini hakufua dafu....huu mkoa ni pasua kichwa...
 
Huu mkoa inaonekana RC kebwe alikuwa na mtandao wake na kwa sasa kila mwana mtandao anajaribu kubeba kile anachoona kinamfaa.

Wakiwabana vizuri wale waliotumbuliwa Kebwe na RAS wake hawatabaki salama, kuna mengi yanasemwa juu ya fedha iliyopotea.
 
haaa haaa umenikumbusha nadhani DR.Rajabu Mtengwe kama sikosei yule alitumbuliwa mkoa wa Katavi akawa analialia rti aonewe huruma sijui kwa alizaliwa kuwa mkuu wa mkoa.Yule alibebwa na JK sijui kapotelea wapi daa siasa bwana.

Haikuwa Katavi Mkuu, ila ni Morogoro
 
Mkoa huu ulishawahi kupata mkuu wa mkoa afisa wa jeshi mstasfu, Brig General Kalembo, lakini hakuweza kuunyosha kisawasawa. Vilevile ulishawahi kupata RC kocha was mpira hsyati Bendera lakini hakufua dafu....huu mkoa ni pasua kichwa...

Inatakiwa ufanyiwe overhaul kuanzia raia wa chini kabisa mpaka wa juu.
 
Jamaa umeeleza vizuri sana! Nimeishi MAHENGE (Kwiro) nimeishi IFAKARA, Madoto - KILOSA, Mkuyuni, Matombo na Kilosa! Unayosema ni sahihi! Mkoa mkubwa na Miundombinu ya bara bara sio rafiki!
Morogoro unatakiwa uongezwe kukatwa Wilaya ili watendaji waaminifu wafanye kazi kwa ufanisi. Mkoa kutoka Moro mjini hadi Kisaki(Mvuha) hakuna lami, Moro mjini - Kilosa lami ya Shida ,Moro Mjini - Malinyi lami inaishia kidatu, Moro mjini -Mahenge(Ulanga) lami inaishia kidatu, Moro mjini - Mlimba lami inashia Kidatu. Mkoa wa Morogoro umekua kama nchi, raia wa upande mmoja hawezi fika upande mwingine kwa urahisi. Unaweza kukaa Matombo (45 km) kutoka Moro mjini, usimuone hata Mkuu Wa Mkoa kwa miaka 10. Kiufupi wafanyakazi wa Serikali Moro Wote ni wapigaji, wavivu na hawakai eneo la Kazi, muda wote wapo Moro mjini wanakula maisha. Kwa mfano wafanyakzi wa Halmashauri ya Mvomero wanakaa Moro mjini, asubuhi ndio wanaenda Mvomero kwa basi, Halmshauri ya Mvua walihama kwa shida na vitisho kwenda mvuha. Washukuru Watu wa Moro wamepoa, na wanajitafutia wenyewe kwa kulima kilimo bila mbolea na madawa, kwahiyo wakulima wa Morogoro, hawana mahusiano makubwa na Tahasisi za Kiserikali, hivyo ata wafanyakazi wakiiba hawaoni athari kwao.
 
ku
Mkoa huu ulishawahi kupata mkuu wa mkoa afisa wa jeshi mstasfu, Brig General Kalembo, lakini hakuweza kuunyosha kisawasawa. Vilevile ulishawahi kupata RC kocha was mpira hsyati Bendera lakini hakufua dafu....huu mkoa ni pasua kichwa...

Kweli Morogoro ni pasua kichwa, pale pana vile viruguru fulani bila kujali ni "Ke" au ni "Me" ni vijizi kupindukia na kama huamini muulize RC wangu Malima, Mama Malechela au waulize madereva wanaotegwa na misumari usiku na kuibiwa, vikikukosa kosa basi katambikie kwani nasikie haviozeshwi mpaka viibe kitu na ndio maana juzijuzi bila aibu vikachomoa betri na kuleta maafa,

Morogoro kuna pasua kichwa nyingine ambayo inaelekea imeshindikana, nikiwa mdogo 1975 naishi Kilosa niliwahi shuhudia mzee mmoja nafikiri alikuwa mkaguru fulani lakini nahisi alikuwa msomi kiasi akihusishwa na ugomvi wa wafugaji na wakulima huko Gairo sikumbuki vizuri jina ila nafikiri alikuwa anaitwa Senyagwa...miaka hiyo mzee huyu alikuwa anamtukana Nyerere acha kabisa, anamtukana kama mtoto wake na kisa ni kwanini karuhusu wamasai wafugaji kuhamia kwao? yeye kulala mahabusu haikuwa shida kwake na nasikia aliwahi kutiwa kizuizini mara kadhaa...sasa mfupa huo uliwashinda ma RC wengi tu achilia mbali huyu Kebwe, KWA UFUPI PASUA KICHWA YA MOROGORO NI SIASA
 
Ule mkoa ilipaswa aondoke kuanzia mkuu wa mkoa hadi mtendaji..pia watu wa halmashauri wangeondoa wote na kuleta wapya ambao sio wakazi wa morogoro
 
Waswahili wana msemo usemao "Sikio la kufa halisikii dawa". RC Mhe. Sanare amekaribishwa Morogoro kwa wizi wa dawa Hosp ya Wilaya Ulanga.

Taarifa hiyo imetolewa na DC Ulanga Advocate Ngollo Malenya mchapa kazi mkubwa,. DC huyu ndiye aliyeibua ule wizi wa zaidi ya 2.9 bilioni Ulanga.

Mhe. Sanare amemuagiza RPC ahakikishe wezi hao wanakamatwa haraka sana. Pia amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama Ulanga kwa kazi nzuri.

Inaonekana kazi hiyo ni 'inside job!!' Sasa sijui kuna mtu alikuwa anaenda kufungua duka la dawa????? Hakuna mahali store imevunjwa!! Wizi ulikuwa very smooth!! Rais Magufuli endelea kuinyoosha nchi. Walizoea hawa.

Mabox hayo yamekamatiwa Mikumi. Viva DC Mhe. Ngollo Malenya. Inyooshe Ulanga walizoea. Huo ndio Mkoa wa Morogoro!! RC Sanare usicheke na nyani!!!!

Queen Esther
Walikuwa wanamjaribu waone makali yake
 
Jana baada ya kukabidhiana ofice mkuu wa mkoa mpya wa Morogoro alipewa taarifa na mkuu wa wiliya moja wapo ya mkoa huo kuna mtumishi mmoja wa moja ya hospitali ya wilaya aliiba mabox 40 yadawa na kuyapakia kwenye basi tayari kwenda kuuzwa Dar lkn habari tunazozisikia ni tofauti kabisa na inasadikiwa kua tukio limekaaa kisiasa zaidi sasa mwenye ukweli atuwekee hapa
 
ku

Kweli Morogoro ni pasua kichwa, pale pana vile viruguru fulani bila kujali ni "Ke" au ni "Me" ni vijizi kupindukia na kama huamini muulize RC wangu Malima, Mama Malechela au waulize madereva wanaotegwa na misumari usiku na kuibiwa, vikikukosa kosa basi katambikie kwani nasikie haviozeshwi mpaka viibe kitu na ndio maana juzijuzi bila aibu vikachomoa betri na kuleta maafa,

Morogoro kuna pasua kichwa nyingine ambayo inaelekea imeshindikana, nikiwa mdogo 1975 naishi Kilosa niliwahi shuhudia mzee mmoja nafikiri alikuwa mkaguru fulani lakini nahisi alikuwa msomi kiasi akihusishwa na ugomvi wa wafugaji na wakulima huko Gairo sikumbuki vizuri jina ila nafikiri alikuwa anaitwa Senyagwa...miaka hiyo mzee huyu alikuwa anamtukana Nyerere acha kabisa, anamtukana kama mtoto wake na kisa ni kwanini karuhusu wamasai wafugaji kuhamia kwao? yeye kulala mahabusu haikuwa shida kwake na nasikia aliwahi kutiwa kizuizini mara kadhaa...sasa mfupa huo uliwashinda ma RC wengi tu achilia mbali huyu Kebwe, KWA UFUPI PASUA KICHWA YA MOROGORO NI SIASA
Kama Serikali inaruhusu wafugaji (wamang'ati, Wamasai, Wasukuma na the likes) kuja Morogoro kufuga mifugo kwenye ardhi ya Wakulima unategemea migogoro haitakuewepo ?. Mungu ameziumba Dodoma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Manyara na Arusha kuwa Mikoa ya Wafugaji kwa kuipa mvua za wastani(chache), na ardhi kavu. Mungu huyohuyo ameziumba Morogoro, Songea, Iringa, Rukwa na Katavi kuwa Mikoa ya wakulima kwa kuipa ardhi na hari ya hewa ya kilimo. Sasa Morogoro ya Wakulima inaletewa Makundi ya Mifugo kutoka katika ardhi za wafugaji, na Viongozi wanangalia tu, toka miaka ya 1980 huko. Leo hii tunatafuta kutatua Migogoro ya wakulima na wafugaji huku tukiendelea kurusu Mifugo kutoka kaskazini kuja Morogoro. Naiomba Serikali ijue kwamba ata Morogoro kuna watu na wazawa wa pale ambao ni wakulima. Kabla ya kuwasaidia wafugaji wageni hapa Morogoro basi haki ya Mkulima wa Morogoro iangaliwe pia. Sasa hivi mifugo ipo mpaka Kisaki(Selous) huko, na wanapanda na mifugo hadi Milima ya Uluguru juu, sasa mito Si itakauka. Sisi wana Morogoro yetu macho(tunawacheki tu). Siku akiingia Raisi mkulima ndipo tutapata haki yetu Morogoro, na siku hizo zinakuja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom