Blessed Jr
Senior Member
- Nov 17, 2016
- 134
- 235
Kuna Video inasambaa ya RC Makonda akiwa Kanisani na anaonekana analia,
Nadhani kulia kwake sio suruhisho la tatizo,
Mimi kama Mkatoliki wakati wa Mafundisho nilifundishwa kuwa, ukikosa omba msamaha nawe utasamehewa.
Haikuishia hapo, nikaambiwa kuwa, ukichukua kitu cha mtu aidha kwa makusudi ama bahati mbaya, unatakiwa uombe msamaha na umrudishie yule uliyemchukulia kitu chake ili asibaki na manung'uniko hata kama atasamehe, kwa kuwa inawezekana ndicho hicho pekee alichokuwa nacho na hakuna namna nyingine ya kukipata.
Makonda anaonekana analia, sawa, lakini kulia kwake kanisani sio msaada kwa kuwa Biblia hiyo hiyo anayotumia ndiyo pengine wanaoitumia aliowaumiza,
Mfano, alisimamia zoezi la wasio na vyeti halali, waliondolewa makazini, wengine wakiwa katika hatua za mwisho za utumishi wao, sisemi walio na vyeti visivyo vyao waachwe, ila kama yeye alijua hana vyeti halali, je, alipata wapi uhalali wa kuwanyooshea wenzake vidole?.
Naamini anaijua na kuisoma Biblia, ikumbukwe kisa cha mwanamke mzinzi, hukumu iliyopitishwa ni kupigwa mawe hadi kufa, lakini Bwana Yesu alisema na makutano yale, aliwaambia kuwa Kama kuna asiye na dhambi miongoni mwao basi awe wa kwanza kumrushia mwanamke yule jiwe.
Kwa kuwa hakuna aliyekuwa mkamilifu, wote wakisita na ndipo Yesu akawaambia, Usihukumu nawe usije ukahukumiwa.
RC Makonda alikuwa mwepesi wa kuwahukumu wenzake, akijua kuwa naye si mkamilifu.
Kwa hiyo asilie, kama Sheria imewekwa ili ituongoze na yeye (Makonda) aliitumia, basi Sheria hiyo hiyo itumike juu yake,
Makonda is not so special kuliko wengine, msumeno ule ule alioutumia basi utumike pia kwake.
Biblia inasema kuwa, kipimo kile kile utoacho ndicho utarudishiwa, kama utaishi maisha yasiyompendeza Mungu usitegemee siku ya hukumu kuiona pepo kwa maana kipimo cha matendo yako ndicho hicho utastahiki.
Warumi 13 inazungumza juu ya kuitii Mamlaka iliyopo,
Makonda ni Mamlaka, lakini Mamlaka aitambuayo Mungu ni Mamlaka iliyojivika utume wa Kimungu, isiyo nyanyasa, onea wala kuwatesa watu wake.
Sasa Mamlaka ya Makomda imekiuka misingi ya Mungu,
Atubu, lakini kama Mamlaka akae pembeni ya Sheria ichukue mkondo.
Kutokuifahamu Sheria haizuii hukumu kwa Mkosaji.
Naamini Mamlaka ya Teuzi inalijua jambo hili ambalo limekuwa likichukua sura mmpya kila siku, sijui kwa nini aidha imeshindwa kumchukulia hatua au kuthibitisha kuwa vyeti vya RC Makonda ni vyake.