Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Kiukweli nakiri kuwa nimeandika uzi huu baada ya kuusoma na kuufuatilia uzi wa Mkuu Lizaboni unaohusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitokeza kesho kwa ajili ya kutolea ufafanuzi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake. Uzi wenyewe ni huu:Paul Makonda kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake kupitia PB ya Clouds FM tar Februari 23, 2017
Inasemwa kuwa RC Makonda ataelezea mambo hayo kupitia Redio ya Clouds kesho. Kimsingi, ingawa wanaozisema nao hawajazithibitisha, RC Makonda ana tuhuma nzito sana zinazoelekezwa kwake. Kuzitolea ufafanuzi, hasa ya kutumia cheti cha sekondari cha mtu mwingine na kuwa na utajiri wenye mashaka, kunahitaji umakini mkubwa.
Kikubwa zaidi, RC Makonda anapaswa kuanika nyaraka za kile ambacho atakitolea ufafanuzi. Mfano,anapaswa kuweka wazi cheti chake cha Sekondari na kuweka wazi hati za mali ambazo anasemwa kuwa anazimiliki. RC Makonda anapaswa kuchambua mambo hayo kwa umakini mkubwa kwakuwa 'jambo laweza kuzua mambo'.
Ndiyo maana nauliza, atakapokuwa akitolea ufafanuzi, waandishi/waulizaji wa habari na hata watu wadadisi watakuwepo? Isije ikawa akatolea ufafanuzi kwa njia ya simu au hata Studioni akiwa na watangazaji wa Clouds tu bila ya kutoa nyaraka zozote. Kama ameamua kuja kutolea ufafanuzi tuhuma/kashfa zake zote, ajipange vyema na kuuanika ukweli.