RC Makonda pigania usafiri jijini

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,803
8,786
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam namheshimu sana kutokana na kuwa na maamuzi ya kimkakati huku mengine yakiwa na matokeo HASI. Mimi napenda kumshauri kwa nguvu kubwa alizonazo kushinda hata mawaziri angelitupia jicho suala zima la usafiri katika jiji hili.

1. USAFIRI WA MWENDOKASI
Huu usafiri ni kama umeshindwa kabisa kutatua kero ya usafiri kwa wakazi wa Kimara Mbezi na sehemu inapopita huduma hii. RC.Makonda toa maamuzi magumu ya kuruhusu haya magari yaanze route ya kutoka Kivukoni mpaka Mbezi moja kwa moja maana kuna magari yanajazana tu pale hata nauli ikiwa Tshs. 1000 hakuna ubaya.

Maana mtu anaweza kutoka Kivukoni kwa Tshs 650 akashukia Korogwe akapanda Bajaj kwa Tshs. 500 jumla ni Tshs 1050. Shauri hawa watu wa huu mradi wa mwendokasi wafanye kutoa mfumo wa usafiri wa daraja la kwanza ambao mtu unaweza kulipia 2000 kwa muda wa asubuhi na jioni kwa kutoka kivukoni mpk mbezi ila gari linakuwa na watu wachache Sasa hawa waendesha mradi huu kipi kinawashinda ebu fanya jambo hapa nakuhakikishia ukitatua kero za usafiri jimbo la ubungo ni lako.

2. URAFIKI NA WAMILIKI WA MABASI
Wewe RC Makonda najua kabisa ni rafiki mkubwa sana wa wamiliki wa mabasi mfano Abood na wengine akina BM unaweza kufanya utaratibu na kuongea nao muda wa asubuhi wakatoa huduma za usafiri maeneo korofi kama Mbagala na Vingunguti kwa pesa hata Tshs 2000 kwa muda wa asubuhi na jioni ili kuondokana na kero za usafiri kila asubuhi na jioni wakatenga magari matano kwa njia hizo mbili na wakafanikiwa kufanya route 5 tu kwa asubuhi na jioni wataweza kupunguza shida ya usafiri sehemu tajawa.

3. COSTA NA NOAH
Hawa wamiliki wa magari wangetengenezewa utaratibu wa kuweza kusaidia kutoa huduma kwa kwa maeneo korofi kwa usafiri hawa wangetengenezea vibali vyao kwa kushirikiana LATRA jiji limekuwa sana na linachangamoto ya usafiri sana.

RC Makonda kwa umakini wako na uchapakazi wako nakuhakikishi jimbo lolote hapa jijini tashinda kwa kishindo kikuu endapo uataweza kutatua kero ya usafiri kwa ufanisi. Wewe ni mwamba hili ni dogo sana kwako.
 
... kama kuna balaa ambalo miundombinu ya mwendokasi imeleta ni kuongeza foleni barabarani! Sasa hivi barabara yote kuanzia Kimara hadi City Centre ni foleni kila mahali kutokana na miundombinu ya mwendokasi; imevuruga kabisa barabara za magari mengine.

Yaani unapunguza tatizo moja halafu unatengeneza tatizo lingine kubwa zaidi! Hivi hao waliotengeneza miundombinu ya mwendokasi akili hazikuwatuma kwamba kuweka zebra kila baada ya mita chache ingetengeneza foleni za ajabu upande wa pili?

Ndio maana ma-V8 na magari mengine binafsi ya viongozi hususan polisi, jeshi, magereza, uhamiaji na wengine "wenye majina" wote wamekimbilia kuendeshea barabara za mwendokasi iwe asubuhi iwe jioni! Kabisa hawakuwaza hilo?

Mimi mwanzoni nilijuwa kwamba kuingia na kutoka kwenye vituo vya mwendokasi vilivojengwa katikati ya barabara ingekuwa kupitia njia za chini ili kuondoa foleni bahati mbaya haikuwa hivyo. Ni muhimu maeneo mengine mwendokasi utakapojengwa (Mbagala, Gongo la Mboto, n.k.) kasoro zilizoonekana njia ya Kimara zisirudiwe. Otherwise, tutakuwa tunatoa magari majumbani kuyapanga barabarani!
 
Back
Top Bottom