RC Makonda na meya wa Kinondoni, Wanachapa kazi kila mmoja kwa namna yake

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Hakika ni huu ni mtifuano mkali na wa aina yake, kati ya mkuu wangu wa mkoa wa Dar es salaam mheshimiwa Paul Makonda na meya wangu wa Kinondoni mstahiki meya Boniface Jacob.

Hawa mafahari wawili wamekuwa ni watu maarufu hapa Tanzania gafla kila mmoja anatimiza wajibu wake na hivo kujizolea umaarufu mkubwa ila nashangaa huyu Jacob kawa maarufu kuliko hata meya jiji zima.

Hakika hii mimi naiona kama ni vita kali kati ya hawa waheshimiwa wawili nawaheshimu sana viongozi wangu na najua mnausoma uzi huu, endeleeni kuchapa kazi kila mmoja kwa namna yake ili jiji lisonge mbele.

NB: Makonda nilikuwa simpendi kabisa kipindi hajawa mkuu wa mkoa, ila kwa sasa nampa salute huyu kijana mwenzetu.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Mitifuano mingine huwa inaleta sana afya kwenye utendaji na afya katika siasa.

Waendelee tu kutifuana aiseee
 
Meya wa Kinondoni kamfunika Makonda vibaya sana.Makonda kabaki na kazi ya uMC wa kuzindua madaraja na kukimbizana na omba omba.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Meya wa Kinondoni kamfunika Makonda vibaya sana.Makonda kabaki na kazi ya uMC wa kuzindua madaraja na kukimbizana na omba omba.
Acha ushabiki wa kipuuzi,,harafu mi ni ukawa mwenzako,ila usikubali siasa ikutawale kiasi hicho
 
Acha ushabiki wa kipuuzi,,harafu mi ni ukawa mwenzako,ila usikubali siasa ikutawale kiasi hicho

Ina maana daraja la Kigamboni (Mwl Nyerere) Makonda alikuwa akifanyakazi gani, Flyover TAZARA Makonda alikuwa MC kila mtu kashuhudia ndio maana may day wafanyakazi walikimbia mkutano wake walinzi wakawanalazimisha watu kubaki majukwaani.
 
Mmmh mkuu wa mkoa umlinganishe na meya wa manispaa? Unazijua protokali kweli wewe?
 
Back
Top Bottom