RC Makonda na balozi wa China waweka jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa bandari, kugharimu $ 450,000

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
389
272
Bila shaka kila mmoja wetu anakumbuka ahadi ya RC Makonda aliyoitoa mwaka jana ya kujenga viwanja vitatu (3) vya mpira kwa ajili ya maendeleo ya mashindano mbalimbali ya michezo ikiwemo Ndondo Cup kwani mashindano haya kwa ujumla wake yanalenga kuboresha mazingira ya michezo na kuzalisha vipaji vingi zaidi ambavyo vinabeba ajira nyingi za vijana ndani yake.

Kimsingi RC Makonda hakuishia tu kuahidi bali alikwenda mbali zaidi na kumualika balozi wa China kushuhudia hali halisi ya viwanja vinavyotumika kwa sasa kama sehemu ushahidi wa kile alichokuwa amemueleza wakati akimshawishi.

Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Balozi kukubaliana na ombi la Mkuu wa Mkoa, leo tarehe 3 Balozi huyo wa China akiwa na RC Makonda wameweka historia mpya baada ya kuweka jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa viwanja hivyo, huku wakianza na kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, huku kikijengwa kwa viwango vya kimataifa na kampuni iliyojenga uwanja wetu wa taifa.

Kuonyesha kutambua utendaji na msukumo mkubwa wa RC Makonda katika kutimiza azma ya Rais John Pombe Magufuli ya kutatua changamoto za wanyonge, Balozi pia amemuahidi Mkuu wa Mkoa kufanya yafuatayo:-

1. Kuwapatia kipaumbele cha ajira vijana wote watakaoshiriki mashindano ya Ndondo Cup kwenye kampuni mbili za nchi hiyo ambazo zinatarajia kuanza shughuli zake hivi karibuni huku wakitarajia kuajiri zaidi ya vijana 24,000

2. Kuipeleka nchini China timu itakayoshinda michuano hiyo ili ikacheze mechi za kirafiki kama sehemu ya kuwaongezea ujuzi wa soka.

3. Kama haitoshi, timu ya pili na ya tatu kwenye mashindano zitapewa mualiko rasmi kwenye ubalozi wa nchi hiyo.

Kwa namna ya kipekee RC Makonda amemshukuru Balozi huyo kwa kuwa sehemu ya watu ambao wamechangia maendeleo ya jiji la Dar es Salaam na hivyo shughuli za maendeleo ambazo hazikuwepo kwenye bajeti ya serikali kuweza kufanya pia.
d18fe9df3ce7fcdab9605d78f2dd9e3a.jpg
 
Chadema walifanya mipango ya kujenga matenity Ward ya akina mama Arusha gambo kaingilia kati eti yy ndo kafanikisha mradi huo na ndio kimepelekea mheshimiwa lema amekaa jela miezi minne!na waliokuwa wanafanya kampeni ili akae ndani muda mrefu ss wamenywea!
 
Dunia ya leo wajinga ndiyo mnaoliwa na mtaendelea kuliwa hakunaga cha bure mjini zaidu ya salamu nyie mnaangalia leo likini mchina kaangalia miaka 13 ijayo tusubiri as time is a best teacher.
Tena ni ujinga wa hali ya juu. Tunashindwa kuwa na dola 500,000 mpaka tukatembeze bakuli? Hii ni aibu. Mimi nataka tuwe na viongozi wanaoona kadhia kuombaomba hata vitu vidogo na badala yake wawe viongozi wa kutuongoza kujitegemea.
 
Huwa ninacheka sana ninapomuona huyo balozi wa China akiwa anapiga picha na viongozi wetu. Sio mara moja au mbili huyo balozi wa China amekuwa akipiga picha na viongozi wetu huku akiahidi miradi kibao, lakini ukiangalia uhalisia hakuna mradi hata mmoja aliotekeleza kama msaada zaidi ya tender wanazopata makandarasi wa kichina. Huyo alipiga mpaka picha kwamba watejenga reli ya standard gauge lakini hela ilikuwa ya mkopo tena ya bank ya kibiashara, na sasa hivi Magu ndio huyo kagoma kuwapa wachina kawapa Waturuki. Alitembezwa mpaka kanda ya ziwa wakati fulani na kina Nape kisha akavalishwa kofia ya ccm ili kuwahadaa wananchi, ikaleta zogo kwa yeye kuingilia mambo ya ndani ya nchi, ccm wakajaribu kukanusha lakini walipobanwa wakajua wamechemka kwani diplomasia haikubali balozi wa nchi kujiuhusisha na siasa za ndani. Huyo Makonda anataka kujifanya ni hao wachina wametoa msaada lakini usikute ni lile kundi lake la ile kampuni iliyompa ardhi huku ikijua ni mali ya serekali, linataka kuendelea kutuia udhaifu uliopo ili kuendelea kujipenyeza. Kwa maneno marahisi huyo balozi wa China ni tapeli na anataka kutumika kama kichaka cha kutakatisha pesa chafu.
 
Back
Top Bottom