RC Makonda asaidia kupatikana kwa I.C.U na emergency unity Wilaya ya Temeke

Malaika Mkuu

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
902
909
Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo amekutana na Balozi wa Japan Nchini Tanzania na kuongelea kuhusu Hospitali zote za Dar, Amana, TMK, na Mwananyamala.

Mhe Makonda amesukumwa na ukosefu wa Emergency unity na ICU ktk hospitali zote hizo tatu.Kwa siku hospitali moja inapokea wagonjwa 1800 hadi 2000 na asilimia 50% ya wagonjwa wanahitaji huduma ya Emergency, Kwa maana nyingine kwa siku niwagonjwa 6000 na 50% ni wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka.

Kwa Kutokuwa na huduma ya emergency kwa hospitali zetu wagonjwa wengi wanakufa na wanaopona ni wale wanaokimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili ambako pia wagonjwa wanapokuwa wengi inakuwa vigumu kuhudumiwa, sababu hiyo ndio imempelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar kukutana na Balozi wa Japan nchini Mh. Masaharu Yoshida ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya Kujenga Emergency Unity pamoja na ICU.

Mhe Balozi amempongeza Sana Mhe Makonda kwa uchapakazi wake na hasa kwakuwagusa wananchi na kumuahidi kumsaidia ujenzi huo ktk Hospitali moja ya Temeke, jambo ambalo limempa matumaini Mhe Makonda kuwa ndoto yake itatimia kwa hospitali zote tatu kwa kuanzia temeke. Mhe Makonda amemshukuru sana Mhe Balozi kwa niamba ya wananchi wa Dar.

1465496167098.jpg

1465496103259.jpg
 
Hii biashara ya zimamoto sijui magamba wataacha lini. Matatizo mengi ya nchi hii hayataisha kwaku solve variable moja. Mfano mzuri ni shule za kata au UDOM saga. Go figure! Magamba acheni umburulaz.
 
Ushabiki tu hapo sasa anapongezwa kwa lipi? kama si kusaka umaarufu wa bei rahis. Emergency unit na ICU is mor thana buildings!
 
Unaomba misaada kwa nchi ambayo haina rasilimali?
Sijui viongozi wetu hawana aibu?
 


Jamaa kwakweli anajitahidi sana na mtu wa kujali safi sana inatia moyo pale kiongozi anapoweka jitihada zake binafsi kujaribu kutatua matatizo ya jamii; I am lost for words safi sana kiongozi.

Subiri sasa uone mitaalamu yetu uchwara iliyo serikarini mwenzao anaweza fanya yote wao wakashindwa kuajiri ili malengo yafikiwe mijamaa hovyo kweli sijui kwanini wengine amuwaoni.
 
Serikali ya makamera ni sawa na mke wako kwenda kwa jirani kuomba akipewa anakuja kujisifu ndani, tuache kuomba omba tutumie rasilimali zetu kuleta maendeleo.
 
Watanzania mtu aliyewaroga ni mtu aliyewanyima elimu, yan hamna akili kabisa. Hivi ulikwisha wahi kujiuliza kwa nin kampuni za bia na soda zinatoa mafridge, matent, viti, mpaka baadhi ya huduma za gharama kabisa bure? sababu wanafacilitate masoko basi. Interest rates Japan ziko chin ya zero, ili kustimulate uchumi, bidhaa ni nyingi hazina wakununua, so wakipata kubwa jinga la kukopa hata kwa interest za juu kidogo, wanaweza kukufanyia chochote ilimradi watabaki na faida. Sasa wakikutana majitu majinga ni kuyapiga tu, mara sijui emergence, mara sijui daraja, mara sijui nin, hii yote sababu akili hatuna.
 
Back
Top Bottom