RC Makonda aimarisha biashara za usiku

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ameanza kufunga taa katika barabara zote za Jiji ili kusaidia biashara kufanyika hadi usiku.

Makonda alieleza mkakati huo wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabishara Tanzania (JWT) katika mkutano wao wa mwaka uliojumuisha wafanyabiashara kutoka mikoa yote nchini.

Makonda ambaye ni mmoja wa wakuu wa mikoa walioapishwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo Machi 15, alisema lengo la kufunga taa ni kuwezesha biashara hadi usiku na kutekeleza kwa vitendo dhana ya Jiji hilo kuwa la kibiashara.

Matukio ya uvamizi wa wafanyabiashara katika sehemu zao usiku kutoka ama kwa majambazi au vikundi vya uporaji kama Panya Road, yamekuwa yakifanya maduka mengi kufungwa mapema jijini.

“Juzi usiku nilifanya ziara ya kukagua taa za barabarani, jambo la kushangaza nilikuta sehemu kubwa ya mji ikiwa ni giza," alisema.

"Hivyo tumeshaanza kufunga taa katika maeneo yote ili kulipendezesha Jiji lakini pia wafanyabishara wafanyebiashara hadi usiku.”

Alisema wafanyabishata walimueleza kuwa wamekuwa wakishindwa kufanya biashara hadi usiku kwa sababu ya kukosa mwanga wa kutosha na kutokuwepo na usalama wa mali zao.

“Ni jambo la aibu wafanyabishara wa Kariakoo wanashindwa kufanya biashara zao hadi usiku… wanalazimika kufunga jioni wakati kuna watu wanatoka kazini usiku na wanataka kununua bidhaa.”

Makonda alisema changamoto zote ameanza kuvifanyia kazi na kwamba atatumia askari polisi zaidi ya 300 wa jiji kulinda usalama wa raia na mali zao.

Source: Makonda aimarisha biashara za usiku | Latest News, Sports, Business, Entertainment, Features, Columnist | IPPMEDIA
 
huyu meya wa dar sijui anafanyakazi gani tangu aapishwe hasikiki kabisa, safi sana makonda ikifika saa mbili ni mwendo wa kufunga barabara na kutandaza viti vya coca cola na tbl kinywaji kwa kwenda mbele,
 
aisee huu ni msaada kwa sisi ambao hatuna muda wa kufanya manunuzi mchana
 
Mi nadhani ni hali ya kawaida tuu kuwepo taa za mtaani usiku au bara barani nakumbuka miaka ya nyuma Temeke hasa wailesi ilikua ina taa za kutosha watoto walifanya kuzivunja..haimaanishi maduka yawe wazi hata huko nje dunia ya kwanza au ya pili taa za kumwaga maduka yanafungwa mapema tuu..
 
ujambazi wa kutumia siraha upo mchana kweupe izo taa za Umeme wa Tanesco si itakua balaa sasa...izo taa ziwekwe ndio maisha tuu hayo ila maduka ulinzi bado usiku..
 
makonda jembe huyu meya naona anaelekea kuwa wa kukaa ofisini na kusubiri taarifa tu.

makonda tengeneza jiji kiwe salama biashara ziwe zinakesha mpaka,asubuhi. ukiingia jioni unafanya manunuzi usiku asubuhi unaondoka zako.
 
Ashirikiane vizuri na madiwani pamoja na meya wa jiji ili kufanikisha malengo yake vizuri maana bila hao fedha ataitoa kwenye bajeti ipi
 
biashara kubwa ya USIKU INAELEWEKA so asante Makonda kuipigia chapuo
 
Asiende na theory! Achana na kuweka maduka wazi hadi usiku ni hatari kwa wanaokuja kununua na wauzaji! Hata aweke askari 1,000 hawezi kudhibiti majambazi! Kama ulinzi waimarishe mchana! Usiku askari waende patrols zao sio kuwatoa patrol wasubiri majambazi kariakoo! Akumbuke maduka yametapakaa mji mzima! Ataweza kulinda kote? Mwenge Tegeta Buguruni etc kote ni business centers!!
 
Sio jambo baya issue na anazifungaje, ina maana kuna fungu la ufungaji taa kwa Mkuu wa Mkoa?
 
kuna njia nyingi za kupata pesa kwa nafasi yake msikariri. anaweza kufanya resource mobilization kwa njia tofauti kuliko mnavyofikiri kwa kutegemea bajeti ya serikali. anaweza kuitisha harambee na watu wakachangia
 
huyu meya wa dar sijui anafanyakazi gani tangu aapishwe hasikiki kabisa, safi sana makonda ikifika saa mbili ni mwendo wa kufunga barabara na kutandaza viti vya coca cola na tbl kinywaji kwa kwenda mbele,
Hata mkibadilishwa ubongo bado hamtaacha kuhangamia kwa starehe
 
kuna njia nyingi za kupata pesa kwa nafasi yake msikariri. anaweza kufanya resource mobilization kwa njia tofauti kuliko mnavyofikiri kwa kutegemea bajeti ya serikali. anaweza kuitisha harambee na watu wakachangia
Bwana Kabila01, sijawahi kukariri katika maisha yangu. Nilichouliza ni anazifungaje? Taarifa haijasema atamobilize resources. Wewe ndio unamjibia au unampa wazo? Na hilo wazo la harambee amelisema yeye au wewe? Mimi sipo kisiasa humu napenda kufahamu means ya utekelezaji. Wewe unaongea resource mobilizatio what is resource mobilization anyway? Which resources are to get mobilized by the Mkuu? What are the priorities maana sifahamu kama la Walimu limeshakamilika tunaenda kwenye lingine. Usirukie baiskeli kwa mbele.
 
Subiri taa ziwake ndo upime kama ni siasa au ni utendaji
 
wa uhakika kariokoo watu wangesha pia

Mtu anatoka mtwara au arusha na gari ya alasiri au jioni anakuja kariakoo anafasha shopping asubuhi au usiku anaondoka kwa maana hata Maduka yangekua na wafanyakazi wa shift pia kama viwanja vya kimataifa huko duniani
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ameanza kufunga taa katika barabara zote za Jiji ili kusaidia biashara kufanyika hadi usiku.

Makonda alieleza mkakati huo wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabishara Tanzania (JWT) katika mkutano wao wa mwaka uliojumuisha wafanyabiashara kutoka mikoa yote nchini.

Makonda ambaye ni mmoja wa wakuu wa mikoa walioapishwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo Machi 15, alisema lengo la kufunga taa ni kuwezesha biashara hadi usiku na kutekeleza kwa vitendo dhana ya Jiji hilo kuwa la kibiashara.

Matukio ya uvamizi wa wafanyabiashara katika sehemu zao usiku kutoka ama kwa majambazi au vikundi vya uporaji kama Panya Road, yamekuwa yakifanya maduka mengi kufungwa mapema jijini.

“Juzi usiku nilifanya ziara ya kukagua taa za barabarani, jambo la kushangaza nilikuta sehemu kubwa ya mji ikiwa ni giza," alisema.

"Hivyo tumeshaanza kufunga taa katika maeneo yote ili kulipendezesha Jiji lakini pia wafanyabishara wafanyebiashara hadi usiku.”

Alisema wafanyabishata walimueleza kuwa wamekuwa wakishindwa kufanya biashara hadi usiku kwa sababu ya kukosa mwanga wa kutosha na kutokuwepo na usalama wa mali zao.

“Ni jambo la aibu wafanyabishara wa Kariakoo wanashindwa kufanya biashara zao hadi usiku… wanalazimika kufunga jioni wakati kuna watu wanatoka kazini usiku na wanataka kununua bidhaa.”

Makonda alisema changamoto zote ameanza kuvifanyia kazi na kwamba atatumia askari polisi zaidi ya 300 wa jiji kulinda usalama wa raia na mali zao.

Source: Makonda aimarisha biashara za usiku | Latest News, Sports, Business, Entertainment, Features, Columnist | IPPMEDIA
Mwambie Ole wao waufanyao ucku kuwa mchana
 
Back
Top Bottom