RC Makonda ahimiza usimamizi ujenzi wa barabara zenye viwango

cocochanel

Platinum Member
Oct 6, 2007
27,309
74,854
unnamed.jpg

MOSHI SHABANI MALLEMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wasimamizi wa miradi ya matengenezo ya barabara kuzingatia taaluma na weledi husika ili kupata thamani ya fedha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu husika bila kukiuka taratibu za manunuzi.

unnamed (1).jpg

RC Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na kuwaomba mameya, madiwani, wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuifuatilia miradi hii kwa karibu, huku akishauri kuwa ni vyema miradi hii ikafanyika kwa gharama nafuu, kwa muda mfupi na kwa viwango, kwani fedha za wananchi ndiyo zinatumika wanapaswa kutendewa haki kwa kuona matokeo chanya kwenye miradi ya maendeleo.

unnamed (2).jpg
[/I]​

Katika hatua nyingine kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited kupitia Mkurugenzi wake Maida Waziri ameeleza kuhusu ujenzi wa barabara zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza kudumu zaidi ya miaka 10, haina vumbi wala uterezi na ujenzi wake hutumia muda mfupi na kuishauri serikali kutumia ujenzi huo wa gharama nafuu kwa takribani asilimia 50, huku akizitolea mfano Australia na Algeria kuanza kutumia ujenzi huo, hivyo hiyo ni suluhu ya lawama za muda mrefu kuhusu barabara mbovu nchini.

unnamed (4).jpg

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa ujenzi huo wa kibunifu utakuwa njia ya kuvifanya vijiji kuwa miji kupitia barabara.

unnamed (6).jpg

Bwana Fabian Campagnolo kutoka kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited , akitoa maelezo kwa wajumbe wa kikao hicho cha barabara , kuhusu ujenzi wa barabara zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza kudumu zaidi ya miaka 10, katika ukumbi wa Arnautoglo


CHANZO; Michuzi blog




 

Attachments

  • unnamed (3).jpg
    unnamed (3).jpg
    30.6 KB · Views: 172
  • unnamed (5).jpg
    unnamed (5).jpg
    34.3 KB · Views: 215
mwenye akili timamu atavaa headphones na kusikiliza muziki popote pale ambapo makonda atakua anahutubia chochote kile iwapo itakua imemlazimu kuwepo kwenye kikao hicho. nihangaike na nalala saa sita sita saba usiku mara nyingine kutoboa kabisa nikitafuta matokeo mazuri ya shule kuanzia olevel, high level, digrii ya kwanza, masters nk leo hii nije nisikilize upuuzi wa mtu aliyefeli lakini akaamua kununua cheti na bado ni kilaza?
 
Back
Top Bottom