RC Kanali Evans Alfred Mtambi: Bajeti ya Elimu chini ya Rais Samia imeongezeka kutoka TZS12bn hadi 232bn VETA 5 mpya zimejengwa ni miaka minne tu.

John John Msakuzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
279
Reaction score
99
==
Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza bajeti ya elimu bure kwa shule za msingi kutoka shilingi bilioni 5.6 mwaka 2020 hadi bilioni 7.5 mwaka 2025, na kwa shule za sekondari kutoka bilioni 6 hadi bilioni 12.85 kwa kipindi hicho, ikionyesha ongezeko la asilimia 34 na 114 mtawalia.

Mradi wa karabati wa majengo ya Kampasi ya Oswald Mang’ombe (MJNUAT) Butiama umeanza tena mwaka 2023/2024 kwa gharama ya shilingi bilioni 2.66 baada ya kukwama kwa takriban miaka 15. Mkoa umepokea zaidi ya shilingi bilioni 85 kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ya elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ikijumuisha shule za awali, msingi, sekondari, Nyumba za walimu na vituo vya walimu (TRC).

Mamlaka ya Vyuo vya Ufundi Tanzania (VETA) imejenga vyuo vitano vya ufundi katika Wilaya za Butiama, Rorya, Serengeti, Tarime na Bunda kwa gharama ya shilingi bilioni 12.71, huku vyuo vinne vingine vikiendelea kujengwa.

Jumla ya shule mpya 27 za sekondari na 20 za msingi zimejengwa au zinaendelea kwa gharama zaidi ya shilingi bilioni 8.6, ikijumuisha Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Mara kwa shilingi bilioni 4.1, Shule ya Sekondari ya Amali Mkoa kwa shilingi bilioni 1.6, na shule tano za sekondari za amali za halmashauri kwa gharama zaidi ya bilioni 2.9.

Ujenzi mkubwa wa miundombinu mpya ya MJNUAT unaendelea kwa shilingi bilioni 102.5 kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaotarajiwa kumalizika mwaka 2025/2026 na kuwaruhusu wanafunzi 1,100 kujiunga katika programu 11 mpya. Jumla ya gharama za miradi yote katika sekta ya elimu mwaka 2025 inafikia takriban shilingi bilioni 231.82 ikilinganishwa na shilingi bilioni 11.6 zilizotumika mwaka 2020, ikionyesha ongezeko kubwa na juhudi za Serikali kuboresha elimu.

1754916966145.png
 
  • Nzuri
Reactions: B47

View attachment 3438421
Tunaelwwa
 
Rais Samia ameibuka kuwa kiongozi shupavu, mwenye dira na maono makubwa kwa taifa letu; ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake ameandika historia mpya kwa kusimamia mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa hekima na busara, huku akilinda amani na mshikamano wa kitaifa; chini ya uongozi wake, Tanzania imeshuhudia kasi ya maendeleo katika miundombinu mikubwa, upatikanaji wa huduma bora za afya na elimu, upanuzi wa miradi ya maji na umeme, ukuaji wa diplomasia ya uchumi na ongezeko la fursa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu; kwa hakika, Rais Samia ni kielelezo cha ujasiri, mfano wa uongozi wa kidemokrasia na taa ya matumaini inayoliinua taifa kuelekea uchumi wa kisasa na maendeleo jumuishi.
 
Kanari mzma anakua chawa akili hamuna afu hawa ndo gwajima anatetea
 
Back
Top Bottom