RC Hapi amaliza mgomo wa daladala Iringa

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
*RC HAPI AMALIZA MGOMO WA DALADALA IRINGA*

*Ni uliotangazwa na madereva zaidi ya 1000*

*Wagoma kukutana na yeyote isipokua Mkuu wa Mkoa*

*Akutana nao,awasikiliza*

*Wampa tano,wasema wanarudi kazini kujenga Iringa Mpya*

Iringa:
Mgomo wa daladala uliotangazwa kwa siku tatu kuanzia jana umemalizwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi baada ya kukutana na madereva hao viwanja vya garden manispaa ya Iringa.
Madereva hao waliogoma kutoa huduma siku nzima ya jana walieleza kuwa hawataki kukutana na uongozi wa manispaa hiyo isipokua Mkuu wa Mkoa kwa madai kuwa manispaa ya Iringa wameshindwa kutatua changamoto zao kwa muda mrefu.
Juhudi za SUMATRA,RTO na Afisa Biashara wa manispaa ya Iringa kwa Madereva hao hazikuzaa matunda yoyote kwani madereva hao walishukilia msimamo wao wa kuwa hawako tayari kuongea nao isipokua Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi.
Baada ya kufika katika viwanja hivyo majira ya mchana (jana jumatatu),RC Hapi alipokelewa na madereva hao kwa shangwe huku wakikaa nae chini ya miti na kumueleza kero zao mbalimbali, wakibainisha kuwa wanataka nao waguswe na “Iringa Mpya” kwa kero zao kufanyiwa kazi kwani wao ni wadau wakubwa wanaomuunga mkono katika kampeni hiyo.

Mkuu wa Mkoa alitumia saa moja kuwasikiliza na kujadiliana nao ambapo kero Kubwa ilitajwa ni kuwa madereva hao wamekua wakinyanyaswa na manispaa ya Iringa, Polisi na SUMATRA huku bajaji zikigeuka kufanya kazi za daladala.
Hapi alitoa maagizo kwa jeshi la Polisi, SUMATRA na manispaa kufanyia kazi haraka changamoto za daladala huku akiwatoa shaka kuwa madereva kuwa atasimamia kuhakikisha wanafanya shughuli zao kwa amani na uhuru bila kusumbuliwa.

Baada ya kikao hicho madereva hao walitoa kauli ya kusitisha mgomo huo na kumshangilia Mkuu wa Mkoa huku wakipiga nae picha.
*Mkoa wa Iringa unazo daladala zipatazo 1000 zinazofanya kazi ya kusafirisha abiria.*

Leo asubuhi daladala zote zimeonekana mitaani kufanya kazi kama kawaida ikiwa ni ishara ya kumalizika mgomo huo.

*IRINGA MPYA*
 
Kumbe hii ndiyo ID yake!
 
Hajamaliza sema katatua kwa leo tu
 
huku bajaji zikigeuka kufanya kazi za daladala


Mawazo mgando, kwani nani kawakataza wao kuhamia kwenye bajaji, hivi mwenye hotel atagoma kutoa huduma ya chakula ati kwasababu mama nitilie naye anauza chakula? Wenye bajaji wanachukua abiria waliokosa nafasi kwenye daladala and not otherwise
 
ktk watu wa baba jesca washamba na limbukeni ni haka kajamaa!,zero brain kabisa
 
Mawazo mgando, kwani nani kawakataza wao kuhamia kwenye bajaji, hivi mwenye hotel atagoma kutoa huduma ya chakula ati kwasababu mama nitilie naye anauza chakula? Wenye bajaji wanachukua abiria waliokosa nafasi kwenye daladala and not otherwise
Wala sio mawazo mgando,
Ukitaka kujua kero ya Bajaji nenda mbeya, mabajaji yanetake over mji wote wa mbeya,
Mji hauna mpangilio, ni hovyohovyo Bajaji zinakatiza kotekote kwa watembea kwa miguu, main road, chocho na kila sehemu, Bajaji nauli ni jero na zikipakia abiria wawili ni mwendo,
Kwa kweli hizo Bajaji hapo iringa ziwekewe utaratibu, hatutaki kuwa na mji kama mbeya,
Tunataka manispaa yetu iwe well organised kama ilivyokuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…