Jim007 2
JF-Expert Member
- Dec 28, 2012
- 395
- 247
Mwekezaji wa kiwanda katika eneo la Kisongo aliyejenga juu ya bomba la maji ameepushiwa hasara kubwa ya kubomoa kiwanda chake na mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo baada ya kujenga juu ya bomba la maji linalopeleka maji katika vijiji vya Loovilukuny, Engorora na Losinoni, hali hiyo imejitokeza leo wakati mkuu huyo wa mkoa alipotembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Kisongo wilaya ya Arusha.
Katika kumweleza changamoto za utekelezaji wa mradi huo wahandisi wa halmashauri walitoa lalamiko lao kwa mkuu huyo wa mkoa juu ya uwepo wa tatizo hilo la kuingiliwa na mwekezaji katika njia waliyotandaza bomba kuu la maji hivyo kukwamisha kumalizika kwa maradi kwa wakati.
Mh. Gambo alitaka kupelekwa eneo husika ili aweze kujionea hali halisi.
Kiwanda kilichojengwa juu ya bomba la maji
Mkuu wa mkoa akitoa maelekezo kwa wataalamu wa halmashauri namna ya kutatua tatizo hilo.
Baada ya mkuu wa mkoa kujionea hali ilivyo alishauri kuwa mwekezaji huyo asivunjiwe bali itafutwe namna ya kuhamisha bomba hilo pembeni na jengo lake na alipie gharama ya zoezi hilo.
Mh Gambo amezindua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa zahanati mbili katika vijiji vya Ilkerin na Ngorora.
Zahanati ya Ngorora
Zahanati ya Ilkerin
Vile vile wananchi na wawekezaji walio katika eneo hilo wamemshukuru sana rais wa awamu ya tano Mh. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuwaondolea kero wananchi wa hali ya chini na wamemuahidi kuendelea kumuunga mkono katika utendaji wake wa kila siku.