RC Dodoma na DED jitafakarini...

Tairi bovu

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
3,063
Reaction score
2,991
Wakuu wa mikoa acheni kutisha watu.
Unasema wasiokuwa na vitambulisho utawafikisha mahakamani ati kwa kukaidi agizo la Serikali?

Wanapelekwa mahakamani kwa sheria na kuvunja au kutenda kosa gani hasa?

Je, si kweli kwamba vitambulisho vya wamachinga ni ghiriba nyingine ya utawala dhidi ya wananchi wake?

Ni wapi duniani kuna kitambulisho ambacho hakina jina? Ni wapi hakuna kinapomuelekeza huyo mtumiaji anatakiwa kufanya kazi wapi na lini?

Je, kwanini wafanyabiashara wanalipa vitambulisho na wakati huo huo wanalipia gharama za vyoo na usafi wa soko.

Bwana Kunambi, DED Dodoma wamachinga wanauliza unawezaje kulipia kitambulisho cha umachinga kisha utoe mchango wa usafi wa soko?

Umejichanganya, ati kitambulisho ni kwa ajili ya meza tu? kwani meza inakaa mbinguni? ama tuseme machinga anaibeba mgongoni?

Mahenge na Kunambi mjitafakari suala la vitambulisho vya machinga ni gumu kulighani hadharani, halighaniki na kueleweka

ALIYETAPELI KOROSHO ZA WAKULIMA NI MHUJUMU UCHUMI KAMA WAHUJUMU WENGINE TU.
 
Kitambulisho ni elfu ishirini tu sawa na sh 50 kwa dei sasa we kelele za nini
 
Ki ukweli inaonekana kama baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wana ugomvi na raia wao au kama wanataka kuwakomoa. There is no harmony.

Mkuu wa mkoa kama atakua na ukaribu na umoja na raia wake kama mkuu wa mkoa wa hapa kwetu Simiyu utakuta kila kitu kinakwenda kama clockwork. No disputes, kodi zinalipwa etc

Mwambieni huyo Mhenge aje Simiyu achukue desa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…