John John Msakuzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 279
- 99
Rais Samia aimarisha Sekta ya Nishati Tabora kwa TZS353.73bn, vijiji vyote 722 vimeungabishwa na Umeme
Katika kipindi cha 2021 hadi 2025, Serikali imetekeleza miradi ya nishati yenye thamani ya TZS bilioni 353.73 mkoani Tabora.
Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuunganishwa kwa vijiji vyote 722 na vitongoji 1,277 kwenye umeme, kukamilika kwa njia ya umeme wa msongo wa KV132 yenye urefu wa km 217 (Tabora–Urambo km 115, Tabora–Sikonge km 102), ujenzi wa vituo vya kupokea umeme Urambo (1x35 MVA) na Ipole (1x15 MVA), utekelezaji wa mkakati wa nishati safi ya kupikia, na usimamizi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki ambapo km 150 zinapita Tabora likiwa na vituo 4 vikubwa.