Rav4 Inapunguza Mwendo ghafla nikiachia Accelerator

mshaurimkuu

Member
Jan 23, 2011
57
30
Mabingwa Salama?

Naombeni msaada wataalamu; nina Rav4 "mpya" (Kili Time ya 2005 ODO reading 63K) inakaribia miezi miwili tangu niitie mkononi kutoka Japan. Ni 4WD; haina gear ya 4WD ila naambiwa ni auto-sense, full-time 4WD.

Hii gari ina matatizo mawili makubwa. Kwanza, accelerator ni nzito kidogo inabidi kukanyaga kwa nguvu. Ukifanya hivyo gari inakamata mwendo. Tatizo ni kwamba, hata kama uko 100kph, ungetegemea ukiachia accelearator, gari ipunguze mwendo taratibu lakini hii sivyo. Inapunguza mwendo ghafla as if umekanyaga breki, unahisi kama gari inavutwa na inasimama ndani ya umbali mfupi sana hata kama uko kwenye mterememko ni hivyo hivyo.

Pili, ukiwa speed zaidi ya 100kph inatoa mlio wa mvumo; inavuma as if kwamba imezidiwa na kwa mfano ku-overtake inabidi nikanyagie kwa nguvu sana kuilazimisha.

Naombeni msaada wataalamu. Shukrani.
 
mcheck fundi mzuri wa umeme! yangu ilikuwa na tatizo kama hilo ilinisumbua sana na mafundi wengi walikula pesa yangu. nilipeleka kwenye computer wakacheck na kukuta kuna shida kwenye control box, inawezekana hizi gari ubovu wake unafanana sana.
 
Shukrani sana kwa ushauri Kiongozi wangu. Nitajaribu kuzingatia ushauri wako.
 
Baada ya swali lako nimetoka kufanya hiyo test Mkuu. Yes; nikiweka D au R bila kukanyaga accelerator itatembea na ilikuwa imepaki kama masaa manne yaliyopita. Shukrani sana Kiongozi for your time.

Swali la mwisho, Je Mfano ukiwa hiyo speed 100 ikianza kujipunguza mwendo huwa mpaka inasimama kabisa au huwa inajipunguza tu na kuanza kwenda mdogo mdogo?
 
Swali la mwisho, Je Mfano ukiwa hiyo speed 100 ikianza kujipunguza mwendo huwa mpaka inasimama kabisa au huwa inajipunguza tu na kuanza kwenda mdogo mdogo?
Kiongozi; inajipunguza na kwenda mdogo mdogo sana hadi naona wa mbele yangu kaniacha kwa mbali ghafla. Sijawahi kuisubiria hadi nione kama itasimama completely ila nahisi nikiiacha itasimama kabisa.
 
Kiongozi; inajipunguza na kwenda mdogo mdogo sana hadi naona wa mbele yangu kaniacha kwa mbali ghafla. Sijawahi kuisubiria hadi nione kama itasimama completely ila nahisi nikiiacha itasimama kabisa.

Gari ipo wapi?

Kama gearbox haina shida. Basi control box inataka reset.

Nilishakutana na Kilitime ambayo ukiaccelerate speed inaishia 10Km/h mpaka uibembeleze ndio speed inaongezeka ila ukiilazimisha haiongezeki. Tulireset control box ikakaa sawa.
 
Gari iko Dar maeneo ya Mbezi Mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom