Rav 4 transimission problem

Rav 4 transimission problem

LEGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
5,122
Reaction score
9,222
wataalam kuna kitu nilikuwa nataka tujalibu kusaidiana hapa juu ya matatizo ya transimission kwenye rav 4 ila tatizo hili hasa lipo kwenye rav 4 kuanzia kwenye family ya S mpaka family ya Z .
ninapo zungumzia familia ya s namaanisha engine za 3s 4s n.k na z namaanisha 1az fe ,1az fse 2az.1nz n.k.

nikwamba haya magari yenye engine hizo ukitembelea kwa mda fulani huwa yanaanza sana kusumbua kwenye mfumo wa gear kama kubadili gear au kustuka na kugonga pindi inapobadili gear.
au kugonga unapo select gear river kutoka p mpaka d.

hapa solution kubwa huwa nikubadili control box na unaweza peleka kwa fundi na akahangaika nayo wee ikatengamaa kwa week 2 au hata mwezi na baadae kama kawa tatizo linarudia tena. ila kwa mjibu wa wao toyota wanadai inabidi ununue control ECM a.k.a ECU nyingine au uwatumie wao wanakwenda kuifanyia servirce,repair then ukija ukifunga inakuwa mkataba.
hapa mm naamini kunamafundi na wataalam wa haya mambo ambao sio mafundi lakini wanaufaham au wanaweza kuingia kufuatilia solution ya hili tatizo na kuja na ufumbuzi.kiukweli mm nifundi nilisha wahikutana na hii ishu na niliwahi solve bila kujua nimesolve vipi zaidi ya kutoa na kubadili baadhi ya IC na TRANSISTOR na kuzi solder tena then tatizo likawa limekwisha.

so kama kuna mtu mwenye ufaham basi wa hata kuwa IC hii au TRANSISTOR,au component yoyote inayohusika na mfumo wa gear hasa zinazo peleka umeme kwenye solenoid valve angetusaidia kutuelekeza hata kwa picha tu.

au ni nini inatakiwa kufanyika ingekuwa safi sana.

na hasa ugonjwa huu umekuwa mwiba na mchungu zaidi kwenye gari ya RAV 4 ya uingereza coz inakuwa na mfumo wa immobilizer.
 
Yaani Kama vile unajua shida niliyo nayo Kaka. Nnayo RAV4 ya kiengereza yenye shida iyo iyo nilihangaika Sana hatimae fundi alinambia nibadilishe control box kitu ambacho Hadi Sasa sijafanya kwa kuhofia pengine sio tatizo Hilo na kuishia kupoteza hela. Msaada zaidi kwa wenye uelewa tafadhali.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom