Ulimakafu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 31,701
- 13,671
Ratiba iliyotolewa na TFF majuzi ya Ligi Kuu Tz Bara, ligi inatarajiwa kutimka hapo Agosti 24 mwaka huu mpaka Novemba 3 itakapo simama kwa takribani miezi mitatu mpaka Januari 25, 2014 mzunguko wa pili utakapoanza.Hivi TFF huwa wanafikiria nini timu kukaa muda wote huo wakiwa mapumziko wengi wakilewa na kucheza ndondo mtaani?Inaovyoonyeaha pia kuna kipindi watacheza mechi mbili ndani ya wiki moja,kwa nini ligi isingeendelea kama vile wafanyavyo England na Ulaya kwa jumla,sana sana wanaweza pumzika wiki 2-3 basi ili wachwezaji wasipoteze 'match fitness'?