RASMI Serengeti Boys Yarejeshwa AFCON

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
226
217
HATIMAYE timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys imerejeshwa kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akiwa mwenye furaha kubwa amesema jioni ya leo; "Timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 17 imefaulu kucheza fainali za Afrika. Hongera Serengeti Boys! Hongera Tanzania!,"amesema Malinzi bila kufafanua.​

Mwanzoni mwa mwezi uliopita, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) liliwapa siku 10 Shirikisho la Soka Kongo (FECOFOOT) kumuwasilisha mchezaji Langa Lesse Bercy mjini Libreville, Gabon afanyiwe vipimo vya MRI ili kuthibitisha umri wake kama anaruhusiwa kucheza mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17.

Katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF jana mjini Libreville, FECOFOOT walitakiwa kumpeleka mjini humo Langa Lesse Bercy akafanyiwe vipimo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya zoezi hilo kushindikana mara mbili.

Na hatua hiyo ilifuatia Rufaa ya TFF dhidi ya mchezaji huyo baada ya Kongo kuitoa U-17 ya Tanzania katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za mwaka huu zilizopangwa kufanyika Madagascar.

Awali, Kongo walitakiwa kumpeleka mchezaji huyo makao makuu ya CAF mjini Cairo, Misri kwa vipimo, lakini mara mbili wakashindwa kufanya hivyo.

source: binzubeir blog
 
serikali nao watie mkono wao hapo vijana waende kambini hata nje ya nchi maana wakiingia kwenye team nne bora watashiriki world cup ya vijana under 17
 
Maneno pekee ya Malinzi tutaamini vipi.. Atuoneshe barua ya uthibitisho iliyokuwa ikisubiriwa
 
Chama cha soka TFF baada yakukata rufaa juu ya mchezaji kijeba wa Congo Brazzaville rufaa hyo Tanzania imeshinda nakupewa nafasi hiyo baada ya Congo Brazzaville kukataa kumpeleka kijeba huyo kufanyiwa vipimo,,,big up Serengeti boys.
 
Kwa hiyo tukishanda tunachukua AFCON ya viboys au
 
Chama cha soka TFF baada yakukata rufaa juu ya mchezaji kijeba wa Congo Brazzaville rufaa hyo Tanzania imeshinda nakupewa nafasi hiyo baada ya Congo Brazzaville kukataa kumpeleka kijeba huyo kufanyiwa vipimo,,,big up Serengeti boys.

Chama cha soka TFF baada yakukata rufaa juu ya mchezaji kijeba wa Congo Brazzaville rufaa hyo Tanzania imeshinda nakupewa nafasi hiyo baada ya Congo Brazzaville kukataa kumpeleka kijeba huyo kufanyiwa vipimo,,,big up Serengeti boys.
 
SERENGETI BOYS YAREJESHWA AFCON, KIJEBA AIPONZA KONGO

Mwanzoni mwa mwezi uliopita, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) liliwapa siku 10 Shirikisho la Soka Kongo (FECOFOOT) kumuwasilisha mchezaji Langa Lesse Bercy mjini Libreville, Gabon afanyiwe vipimo vya MRI ili kuthibitisha umri wake kama anaruhusiwa kucheza mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17.
Katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF jana mjini Libreville, FECOFOOT walitakiwa kumpeleka mjini humo Langa Lesse Bercy akafanyiwe vipimo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya zoezi hilo kushindikana mara mbili.
Na hatua hiyo ilifuatia Rufaa ya TFF dhidi ya mchezaji huyo baada ya Kongo kuitoa U-17 ya Tanzania katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za mwaka huu zilizopangwa kufanyika Madagascar.
Awali, Kongo walitakiwa kumpeleka mchezaji huyo makao makuu ya CAF mjini Cairo, Misri kwa vipimo, lakini mara mbili wakashindwa kufanya hivyo.
Fainali za U-17 Afrika ilikuwa zifanyike nchini Madagascar kuanzia Aprili mwaka huu, lakini mwezi uliopita CAF iliivua uenyeji na kutoa muda hadi Januari 30 mwaka huu nchi nyingine kujitokeza kuomba uenyeji.

Similar Discussions

Back
Top Bottom