GE2025 Rasmi: Pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mpina lakubaliwa. Tume yamnyoa, ACT yakosa mgombea urais

GE2025 Rasmi: Pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mpina lakubaliwa. Tume yamnyoa, ACT yakosa mgombea urais

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
440
Reaction score
3,211
Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Ndugu Hamza Saidi Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Hivyo, jina la Ndugu Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Aidha, mapingamizi yaliyowekwa wa Mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan yametupiliwa mbali.

Soma Pia: Mpina ashinda kesi kuenguliwa kuwa mgombea Urais

Pia soma: Mgombea Urais ACT, Mpina awekewa mapingamizi ya uteuzi wake na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Wagombea Urais NRA na AAFP

1000444068.jpg

1000444070.jpg
1000444069.jpg
 
KUHUSU UAMUZI WA PINGAMIZI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA WA KITI CHA RAIS KWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
DAR ES SALAAM, Tarehe 15 Septemba, 2025

Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 37 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 kikisomwa pamoja na kanuni ya 22 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, tarehe 13 Septemba, 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea jumla ya mapingamizi matatu (03) dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo na tarehe 14 Septemba, 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea pingamizi moja (01) dhidi ya uteuzi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Tume katika kikao chake kilichofanyika tarehe 15 Septemba, 2025 imefanya uamuzi wa mapingamizi hayo manne (04) yaliyowasilishwa mbele yake, ambapo mapingamizi matatu (03) yamekataliwa na moja (01) limekubaliwa kama ifuatavyo:-

1. Mapingamizi yaliyokataliwa
Tume imekataa na kuyatupilia mbali mapingamizi matatu (03) kama ifuatavyo:-

i. Pingamizi lililowekwa na Ndugu Almas Hassan Kisabya mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha NRA dhidi ya Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa Kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo

Tume imekataa na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na Ndugu Almas Hassan Kisabya mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha NRA dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

ii. Pingamizi lililowekwa na Ndugu Kunje Ngomale Mwiru mgombea kiti cha Rais kupitia chama cha AAFP dhidi ya Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa Kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo.

Tume imekataa na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na Ndugu Kunje Ngombale Mwiru mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama AAFP dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

iii. Pingamizi lilowekwa na Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea kupitia Chama cha ACT-Wazalendo dhidi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Tume imekataa na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na Ndugu Luhaga Joelson Mpina dhidi ya uteuzi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

2. Pingamizi lililokubaliwa
Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Ndugu Hamza Saidi Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Hivyo, jina la Ndugu Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

"KURA YAKO HAKI YAKO JITOKEZE KUPIGA KURA"

M1.jpg
m2.jpg
m3.jpg
 
Tume yenyewe eti Mwenyekiti na mkurugenzi wake wanateuliwa na mwenyekiti wa ccm! Yaani wanajiamulia tu wenyewe wampitishe nani kugombea, wamuache nani, au wamtangaze nani kuwa mshindi!

Kwa kweli huu ujinga hauvumiliki hata kidogo.
 
Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Ndugu Hamza Saidi Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Hivyo, jina la Ndugu Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Aidha, mapingamizi yaliyowekwa wa Mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan yametupiliwa mbali.

View attachment 3472514

View attachment 3472515View attachment 3472516
Ilikuwa ngumu kumruhusu apande jukwaani kumnanga malkia
 
Hayo tuliyajua muda mrefu

Huyo Mpina hajui kwamba timu yetu inataka ushindi wa asilimia 99

Na yule mgombea kutoka CAT pale mwisho wa reli, ndiyo atakuwa Mbunge Pekee kutoka upinzani Mwaka huu maana ndiyo mtoto pendwa wa Mama
Usitake kunambia Mpina hayajui yote haya.
 
Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Ndugu Hamza Saidi Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Hivyo, jina la Ndugu Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Aidha, mapingamizi yaliyowekwa wa Mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan yametupiliwa mbali.

View attachment 3472514

View attachment 3472515View attachment 3472516
nilifikri ni fake news nime scan code kumbe ni official aiseeeee
 
Usitake kunambia Mpina hayajui yote haya.
Hakuwa anayajua

After all, ACT imekuwa Chaguo la 3 la Mpina baada ya CCM na CDM

Mwanzoni Mpina alikuwa aende CDM iwapo ingeshiriki Uchaguzi huu

Ndiyo maana alianza kuvaa nguo zinazo shabihiana na Kombati za CDM zile nyeusi
 
Back
Top Bottom