Rasimu ya Katiba; 21 (1)

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,435
3,182
Nanukuu 'Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine ya malipo ya mshahara'.
Ibara hii inaweza kuwa nzuri sana kwa kuwa itajenga mazingira ya watu wengi, hususani vijana, kupata ajira, pia waajiri kuheshimu makubaliano.
Ila napata wasiwasi kidogo, kwa mfano, ikiwa kama madaktari hawatafanya kazi za ziada katika hosptali binafsi, ili hali hakuna madaktari wa kutosha, kisha huduma za afya katika hosptali binafsi, ambazo ni msaada mkubwa sana kwa serikali, kudorora, je Rasimu hii, kwa Ibara hii, itatuganga magonjwa?
Mtizamo wangu: Kuna baadhi ya taasisi, hususani zenye wafanyakazi, ambao ni wachache na ambao ni vigumu kuwaanda kwa muda mdupi, kuruhusiwa kwa utaratibu maalumu kufanya kazi za ziada katika taasisi binafsi kwa maslahi ya wengi.
 
Back
Top Bottom