Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 579
Wadau,
Nilikuwa katika usomaji wa rasimu iliyopendekezwa na tume na nimeona kama ibara hizi mbili zinapingana na pengine wataalamu wanisaidie tafadhali. Nanukuu kutoka katika Sura ya Tano, Serikali ya Shirikisho. Ibara nionazo kama zinapingana zipo katika Ibara ya 36, ibara ndogo za (3) na (5):
(3) Ikitokea kwamba kiti cha Rais kiwazi kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmojawapo na wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani:-
(a)Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi
(b)Waziri Mkuu na kama nafasi yake iwazi au kama nayeye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(c) Gavana wa Tanganyika au, Zanzibar kwa mlolongo huo;
(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au akili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Waziri Mkuu wa Shirikisho ataapishwa na atakuwa Rais na uchaguzi wa Rais utafanyika ndani ya miezi mitatu isipokwa tu pale ambapo muda wa Bunge uliobakia hauzidi miezi sita uchaguzi wa Rais utasubiri uchaguzi mkuu;
Eneo nionalo linapingana ni lile ambalo katika ibara ndogo ya (3) madaraka ya Rais (ikiwa kiti cha Rais kiko wazi) yanahamishiwa kwa Makamu wa Rais (kabla yakuangalia mlolongo mwingine). Lakini katika ibara ndogo ya (5) anayeapishwa kushika nafasi ya Rais (ikiwa kiti cha Rais kiko wazi) anakuwa Waziri mkuu wa Shirikisho. Je, ibara hizi mbili hazipingani kweli. Wataalamu tafadhalini tupatiane uchambuzi.
Jambo lingine, naona kumekuwa na typos (spelling errors) nyingi sana katika rasimu hii, hasahasa katika matumizi ya maneno "Jamuhuri" na "Jamhuri". Je ikiwa hii ndo ingekuwa ni katiba rasmi, mapungufu haya hayana athari za kisheria?