RASIMU Ibara 39 Ibara ndogo ya 3

RASIMU Ibara 39 Ibara ndogo ya 3

Mtumbatu

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2012
Posts
363
Reaction score
171
Ibara ya 39 Ibara ndogo ya 3

(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake.

Hii ina mana baada ya rasimu hii kupita tutaifanyia marekebisho sheria ya ugaidi au ... sheria hiyo itakuwa ya Tanganyika na Tanzania mpya itaunda sheria nyengine kukidhi matakwa ya katiba?
 
Ibara ya 39 Ibara ndogo
ya 3

(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote
kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa
yake.

Hii ina mana baada ya rasimu hii kupita tutaifanyia marekebisho sheria
ya ugaidi au ... sheria hiyo itakuwa ya Tanganyika na Tanzania mpya
itaunda sheria nyengine kukidhi matakwa ya katiba?
Mpango wa kuepusha watu kwenda The Hague
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ha ha haa! Sheria hiii safi sana, sisi kama Marekani vile, we are no longer members wa ile mahakama inayoshughulikia viongozi wa africa.
 
hii inaweza kuwa nzuri na mbaya kwa upande mwingine....
 
siungi mkono hii hoja sababu nahisi kuna agenda ya siri nyuma hii hoja.
 
Duh! Inamuepusha jamaa naa yele yaliyotokea hadi kufikia hatua wana harakati wakapeleka mashtaka the hague
 
Warioba anamtengenezea swaiba wake mazingira ya kukwepa mkono wa sheria za ulimwenguni ambazo yeye mwenyewe kazishabikia sana kuhusu haki za binadamu. Wajanja kweli hawa jamaa. Siungi hoja hiyo ng'o!
 
Ibara ya 39 Ibara ndogo ya 3

(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake.

Hii ina mana baada ya rasimu hii kupita tutaifanyia marekebisho sheria ya ugaidi au ... sheria hiyo itakuwa ya Tanganyika na Tanzania mpya itaunda sheria nyengine kukidhi matakwa ya katiba?
Tusije kugeuka kuwa hifadhi ya wahalifu! Nadhani kuliacha suala hilo kuwa ridhaa ya muhusika sio sahihi. Pengine ingekuwa bora kama uamuzi wa kumpeleka ama la ufanywe na mahakama ili kuweza kusikiliza hoja za mtuhumiwa ambaye anatakiwa nje ya nchi.

Vipi kuhusu mikataba mbalimali ya kimataifa ambayo tumeingia itakuwaje?
 
suala hili linahitaji umakini wa hali ya juu kwa sababu wakati mwingine hawa watawala wanapokuwa madarakani hujisahau na kujiona kama miungu watu au israil mtoa roho za watu wao hivyo kama tutasema hvy ktk katiba basi ktk sheria itafutwe namna ya kuwawajibisha humu humu nchini pale tutakapoona kwa makusudi mazima kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
 
Hujui kuwa baadhi ya wakubwa wetu wana mashaka ya kushitakiwa the Hague? lazima wajenge mazingira ya kuepuka hilo. Lakini pia kuwa na mfumo wa mahakama mzuri wenye kuweza ku-address hilo inafaida kwa nchi.
 
Back
Top Bottom