Rasilimali zilizopo zinavyoweza kulikomboa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rasilimali zilizopo zinavyoweza kulikomboa Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 21, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 21.10.2008 0004 EAT

  • Rasilimali zilizopo zinavyoweza kulikomboa Taifa

  Na Glory Mhiliwa
  Majira

  BALOZI wa Marekani hapa nchini Marc Green na mwaharakati wa haki za Wamarekani weusi nchini Marekani Mch Jesse Jackson ni miongoni kati ya watu kutoka Bara la Ulaya kuhoji Tanzania kuwa masikini.

  BALOZI Marc Green anasema kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha kuwa inasonga mbele kimaendeleo kwa kutumia rasilimali zake ipasavyo.

  Anasema kuwa Tanzania ni mojawapo kati ya nchi zilizo nyuma kimaendeleo hata orodha ya nchi masikini duniani inathibitisha hilo.

  'Tanzania ni nchi ya 159 ya kimasikini kati ya nchi 177 orodha hii inaonesha kuwa Tanzania ipo mwisho kabisa zinahitajika juhudi katika kuondoka mkiani na kufikia kileleni," alieleza Balozi Green.

  Balozi Green anasema kuwa kama Tanzania inampango madhubuti wa kuondokana na umasikini kuna haja kwa Tanzania kutumia ipasavyo rasilimali zake ili kuliwezesha Taifa kuondokana na umasikini.

  Anatanabaisha kuwa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kwa kuwa na udongo mzuri unaofaa kwa kilimo na wenye rutuba nzuri na mvua zinazonyesha kwa wakati.

  "Kilimo chenyewe kinaweza kulipatia Taifa hili maendeleo ukiachilia mbali sekta nyinginezo kama sekta ya madini ama viwanda, udongo wa Tanzania bado unarutuba inayofaa kwa kustawisha mazao tofauti na nchi nyingine ambazo udongo wake haufai kwa kilimo," anasema Balozi Green.

  Anasema kuwa ikiwa kilimo kitapewa kipaumbele zaidi kinaweza kutosheleza mahitaji ya ndani na sanjari na soko la nje hususani kwa baadhi ya mazao kama vile zao la kahawa ambalo likiboreshwa litaweza kuongeza kasi ya mauzo kwa nje ya nchi.

  Akizungumzia sekta nyingine ambazo nazo zikitumika ipasavyo kwa maslahi ya Taifa Balozi Green anasema kuwa sekta ya madini ni sekta ambayo inaouwezo wa kuifikisha mbali Tanzania lakini kama sekta hiyo itatumika kama kiongozi wa maendeleo ya kiuchumi.

  Anasema kuwa ni muhimu kwa manufaa ya vizazi vijavyo mikakati endelevu ya kukuza uchumi wa Tanzania ikaanza kuchukua sura mpya kuanzia sasa hivi.

  Naye Mwanaharakati wa haki za Wamarekani weusi Mchungaji Jesse Jackson katika kipindi cha mkutano wa Leon Sullivan ambapo alishiriki ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea Tanzania aliungana na Balozi Green katika kuitaka Tanzania kutumia rasilimali zake ipasavyo ili kuweza kuondokana na umasikini.

  Mchungaji Jesse anasema kuwa kupitia mkutano wa nane wa Leon Sullivan ameweza kutembelea eneo la maajabu ya nane ya Dunia ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kubaini kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi za kuiwezesha kuondokana na umasikini.

  Anasema kuwa Ngorongoro ni mahali pekee duniani ambapo panaonesha historia ya binadamu wa kale waliokuwa wakiishi kwenye bustani moja wanyama binadamu bila ya kudhuriana.

  "Dunia nzima hakuna mahali ambapo utakuta binadamu na wanyama wanaishi kwa pamoja bila ya kudhuriana tena wanachangia maji kwa pamoja hii inatukumbusha historia ya kwenye biblia ya bustani ya Edeni, anasema Mchungaji Jesse.

  Anasema Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ndiyo Eden hai iliyopo duniani na hakuna mahala pengine inapatikana zaidi ya Tanzania ingawa haifahamiki kama ilivyo na umuhimu kwa Dunia nzima.

  Alieleza kwake kuushangazwa na Wamasai kuishi kwa pamoja na wanyamapori, mifugo ya Wamasai kula kwenye malisho ya pamoja na wanyamapori bila ya kudhuriana wakati maeneo mengine binadamu na wanyamapori ni maadui.

  Aliitaka Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika hifadhi zote kama ilivyo kwa NCAA hali aliyoelezea kuwa itachangia katika kuongeza kiwango cha watalii kwa mwaka wanaotembelea vivutio vya Tanzania.

  "Hiki ni kigezo tosha kwa kuwaleta watalii wengi kuja hapa Tanzania kutembelea hifadhi hii ambayo yenyewe inaouwezo wa kuendesha uchumi wa Taifa hili," Mchungaji Jackson anaelezea maoni yake.

  Alieleza kuwa Tanzania inatakiwa kujitangaza zaidi ili mataifa kutoka nchi zilizoendelea kama Marekani na China kufahamu vivutio vilivyopo Tanzania hali itakayosababisha kuongezeka kwa watalii watakaokuwa wakitembelea hifadhi za hapa nchini.

  Hata hivyo Mchungaji Jesse alisema kuwa Tanzania inajivunia kuwa na vivutio vingi vya wanyama kuliko nchi nyingine yoyote Barani Afrika.

  Anasema kuwa kupitia rasilimali wanyama Tanzania kimapato inao uwezo mkubwa wa kusonga mbele zaidi kiuchumi kupitia mapato ya watalii wanaotembelea hifadhi hizo.

  "Hifadhi za wanyama Afrika zipo nyingi zikitumika ipasavyo zenyewe zinatosha kabisa kuliondoa bara la Afrika katika lindi la umasikini lakini kama vitatangazwa na nchi zilizoendelea kuvitambua," anasema.

  Hata hivyo alisema kuwa nchi yake ya Marekani kwa mujibu wa Kaimu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw Benard Murunya ndiyo inayoongoza kwa raia wake kutembelea hifadhi hiyo.
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa sababu tu ya natural resource (mali asili) kilichosababisha nchi nyingi kuendelea ikiwa pamoja na zile ambazo hazina mali asili kama (Switzerland) ni "RASILI MALI WATU" Human Resources...

  It is not about how many but the quality of human resources.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kama wapo wale ambao hawakutegemea mali asili nasi tukajikuta tunazo nyingi kupindukia; sasa tumekwisha jiuliza, je wao walitunikiwa vipi hizo "raslimali watu" ili tuweze kuleta uwiano baina ya hivi viwili na kutusukuma katika maendeleo tunayoongelea?

  SteveD.
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwanza

  Tuanze na kufanya self assessment, tujitambue kwanza sisi tuna strength gani? na Weakness gani? Hivyo tu-develop human resources capacity kwenye nyanza muhimu za uchumi

  Pili

  Tuwaelimishe wananchi kwa kampeni kubwa ya kitaifa kwa lugha rahisi ya kueleweka kwamba ile tuendelee tuanze wapi na tuishie wapi!

  Tatu
  Tuwe na SMART objectives and goals... Simple Measurable Attainable, Relialistic and Time based.

  Nne
  Tuweke legal framework ya kupima mafanikio na changamono na kuwa na dynamic system ya ku-correct mambo kwa wakati.

  Tano:
  Tusherekee mafanikio na kuzawadiai watendaji wazuri na kuwapa nishani mbali mbali kwa mfano.
  - Nishani ya Rais iliyotukuka kwa kuweka mfumo wa kuondoa foleni Dar.
  - Nishani ya Jamhuri... hii inakuwa kubwa kuliko zote
  _Nishati ya Bodi za Proffesional etc.
   
 5. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ulioyoongelea hapo juu nayakubali, lakini nilitaka kuongezea tu kuwa nadhani zipo nchi ambazo zimetumia rasilimali ili kuendelea as 'a starting point'. Nchi nyingi za ghuba zinategemea au zilitegemea mafuta ambayo ni rasilimali kama ilivyo almasi, dhahabu, rubi, ardhi na kadhalika katika kuongeza kasi ya maendeleo yao, ila nadhani tofauti ni jinsi gani viongozi wanaopewa dhamana ya kusimamia hizo rasilimali wanawajibika kama inavyotarajiwa kwa manufaa ya watu wote.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Naam, nchi hizo mojawapo ni Venezuela ambako rasilimali za Taifa hilo zinatumika katika kuinua viwango vya wananchi wa nchi hiyo, ingawaje matajiri wa nchi hiyo wanapinga hilo. Sisi pia rasilimali zetu zinaweza kutumika vizuri ili kuinua viwango vya maisha vya Watanzania walio wengi, badala ya kuendelea kupata asilimia tatu tu kwa mfano toka mapato ya dhahabu yetu. Nchi yoyote duniani kamwe haitakubali ipate asilimia tatu tu toka rasilimali zake, isipokuwa Tanzania.
   
Loading...