Rasilimali za Tanzania zazidi kutafunwa: JK achekelea tu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rasilimali za Tanzania zazidi kutafunwa: JK achekelea tu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Informer, Dec 16, 2010.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwezi Mei mwaka huu, Kikwete alienda Serengeti kupokea vifaru watano waliokuja kwa ndege kutoka Afrika Kusini huku akichekelea kama kawaida yake. Akiwa huko Serengeti, alikutana hotelini na rafiki yake mbunge Lazaro Nyalandu akiwa ameongozana na mamiss. Kikwete hakurudi Dar siku hiyo akalala hotelini Serengeti. Nyalandu sasa ni naibu waziri.

  Hiyo ni chombeza tu, lakini issue hapa ni kuwa kifaru mmoja kati ya watano waliokuzwa kwa gharama kubwa Afrika Kusini na kusafirishwa kwa ndege mpaka Tanzania kauliwa na majingili.

  Hii ina maana kuwa serikali ya Kikwete inashindwa kulinda rasilimali za nchi. Mimi naona bora hao vifaru wabaki huko huko Afrika Kusini mpaka WILLIBROD SLAA akiwa Rais 2015 na kuunda serikali makini itakayotunza vizuri rasilimali za taifa.

   
 2. T

  The Informer Senior Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Naililia nchi yangu Tanzania!!!!
   
 4. m

  mams JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hao walio uwawa ni kwa sababu mnawakumbuka walikuwa watano. Ni wanyama wangapi msio na hesabu yao wanateketea.
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Kukukumbusha tu Dr,alisema anagombania nafasi ya Urais mara moja tu.

  Hili la kuuawa kwa wanyama ni katika mlolongo tu wa mambo mengi ambayo katika Tanzania yetu yanatufanya tuwaze sana na kupata mvi kwa haraka.

  Watu,wananchi wengi wanakufa, wanauliwa ovyo ovyo tu,mahospitali kwa ukosefu wa dawa na zana za matibabu. Barabarani kutokana na kutozingatiwa kanuni za kutumia barabara, ujambazi na kwa umaskini kwa ujumla.

  Kwa hiyo hapa TZ kila kitu kinauliwa, juzi juzi nimesoma vigogo wanauwa miti Mufindi. Kwa hiyo kifo kimetuzunguka, bandugu !
   
 6. D

  DENYO JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa faida ya wale ambao hawakuipata TAARIFA KAMILI YA CHADEMA
  Najua kuna wengi huenda hawakuipata hii. Nimeitafuta sijaiona jamvini baada ya rafiki kuniambia niitafute. Ila nimeikuta feacebook yake. Wanaoitafuta kama mimi, hii hapa

  Msimamo wa Chadema haujabadilika

  by Dr. Wilbrod Slaa on Tuesday, December 14, 2010 at 7:29pm  Kuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa Chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

  Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

  Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".

  Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, Chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina Mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili Tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa Katiba na Sheria mbovu kama tuliyonayo leo, Chadema inasisitiza upatikanaji wa Katiba mpya, Shirikishi na ya Wananchi.

  Upatakanaji wa Katiba hii utakuwa na mchakato, na kama Serikali haitaki, basi Chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi Katiba ya Wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

  Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa Taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na Busara daima huvuta heri.
  Source: Gonga hapa Msimamo wa Chadema haujabadilika | Facebook


  NYONGEZA: Kuna thread imewekwa hapa chini na Mwanajamii mmoja (Chapakazi) anauliza tofauti ya maneno haya mawili (Lawful na Legitimate). Kwa uelewa wangu. Naomba niiongeze hapa kwa mtiririko sahihi. Unaweza toa usahihi zaidi


  Moja ya tafsiri za legitimate zilizoko kwenye link hii define: legitimate - Google Search


  Zinasema kitu
  legitimate ni kile ambacho kiko affirmed to be just na in accordance with recognized or accepted standards or principles.


  Na kitu
  lawful ni kitu ambacho kiko recognized or sanctioned by law(lawful: meaning and definitions — Infoplease.com.


  Kwa upeo wangu hii inamanishaa kitu kinaweza kuwa recognize na sheria lakini kisiwe just kwa sababu hakikiendana na accepted principles  Tukitumia mfano wa tukio lenyewe naweza kusema hivi,

  Sheria inasema Raisi ni Raisi kwa kutangazwa na tume (lawful) lakini ili atangazwe lazima kanuni (principle) kadhaa zifuatwe.


  Hivyo kama kanuni hazikufuatwa lakini katangazwa (kama sheria inavyotaka) na tume ya uchaguzi basi ni lawful kwa sababu katangazwa kisheria na tume yenye mamlaka ya kisheria kutangaza lakini kama kanuni za kufuatwa ili atangazwe zimevunjwa tunasema ni illegitimate kwa sababu principle s zimekiukwa.


  Kwa msaada zaidi gonga hili link uone mfano kule Georgia

  http://georgiandaily.com/index.php?o...2829&Itemid=68
   
Loading...