Ramadhani Singano "Methi" anafanyiwa hujuma ama amepata alichotaka Azam?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
7,869
16,913
tunakumbuka mwaka jana kwa sisi tunaofatilia mpira suala lake la mgogoro na simba sc. katika michezo lilikuwa gumzo la namna yake kuhusiana na suala lake la kughushiwa saini n.k lilienda lilivyoenda hatujui wat happened ila tunajua mwishoni ramadhan singano alifanikiwa kusajiliwa azam.
sitaki nizungumzie suala la ule mgogoro kwa sababu ukweli unabaki kuwa kwao. mimi nlikuwa na bado naangalia maslahi ya huyu kijana ambaye tungejiuliza kabla ya simba alitoka wapi na kufika pale? wengi wanasema ana kipaji nami sikatai nlitaman sana kumwona awe ni mchezaji anawefanya vizuri kwa ajili yake mwenyewe kwanza na badaye taifa lake. kwa team yoyote ambayo angechezea. najiuliza je alikuwa emaiva kuwa na mbwembwe na migogoro ile ywa kwenye vyombo vya habari na club ya simba? ilikuwa na tija kwake? nani alikuwa mshauri wake? huko aliko kumemsaidia kukuza kipaji chake? sijamsikia kwa kipindi kirefu kidogo lakini pia ningependa ili liwe somo kwa wachezaji wa timu yoyote kama upo club flan ukajihakikishia namba na uwezo wako bado haujawa mkubwa usiriushe mateke. si ajabu sinagno amecheza mechi chache sana akiwa azam na je anaonekanaje kule azam? ni yule yule ramadhan singano messi au methi?
kuna wadau wanaoweza kuwa na tarifa nyingi kuhusu huyu bwna mdogo ambaye pamoja na yote binafs nlimwona alikosa busara au ushauri umzuri angeliendesha hili suala kimichezo na kulimaliza kimichezo then angeweza kuendelea vyema na kipaji chake. nawashauri wachezaji kama umebebwa na team usirushe mateke ikiwa bado hujakomaa kuweza kukimbia wenyewe safari ndefu.
azam tunawataka mumchezeshe singano mechi nying msiue kipaji chake. au mlikuwa na lengo gani naye? na je anapopangwa anapata ushirikiano mzuri uwanjani? tunataka kuona messi wetu akifanya vizuri zaidi na zaidi.
 
Ni
Singano amekua ni darasa zuri sana kwa vijana wenzake.
kweli bandugu, ila sidhhani Kama wanasikia, waandishi nao wanachochea, walipiga picha anachoishi cha kaka. Take huku wakishare kitanda. Ajabu Kuna watu wanamshahara wa laki tatu Na wanajitegemea, sembuse kwenye laki sita Na gari ya kazi Suzuki Kerr.
 
Ukiangalia utajua bwana mdogo hana akili nzuri, anapata ushauri mbaya au kuna mtu anamtumia. Kusema ana lala kwa kaka yake anapata salary ya 600,000 na posho pia na bado ana gari ya kazi ambayo hata ikimwingizia 10,000 kwa siku ni nying.halaf bado analala kwa kaka yake basi anaonesha bado ni mjinga.alikuwa na nafasi ya kuomba pesa ipande au kujipanga atoke vipi. Sijajua kwa sasa anaishi maisha gani na anapata tsh ngap.lakini je kwa umri wake mpira unaendeleaje?Je ameshafikia malengo?alipaswa kupata ushauri mzuri ataua kiwango chake cha mpira na kuna siku atatemwa huko aliko.kuna mwanamichezo anayeweza kutwambia huko aliko amecheza mech ngapi sasa na yukoje na yukoje uwanjan?

Wa kulaumiwa ni Shaffih Dauda ambaye kila mara alikuwa akijaribu kushawishi wasomaji wa blog yake kuwa Methi anaonewa. Nakumbuka kulikuwa na mfululizo wa makala kule, mara Singano anakaa gheto kwa kaka yake, mara analipwa mshahara kidogo, mara anashea kitanda na kaka yake! Yaani kulikuwa na makala nyingi hadi akawa anaandika INAENDELEA KESHO! Sehemu ya makala katika blog hiyo ni hii:
SINGANO AKISHINDWA KUMALIZANA NA SIMBA KATIKA MAZUNGUMZO MPYA ITAKUWAJE?

Kama TFF wamewataka Singano na Simba kuzungumza upya kwasababu mikataba yote imefutwa, maana yake wakishindwana, Singano anachukua hamsini zake na sio lazima akubali kuendelea kuichezea Simba.

Wakati huo huo, mtandao huu umefahamishwa kuwa, Katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa amemuandikia barua Singano ambayo nakala yake amechukua mwenyekiti wa SPUTANZA, Bwana Kisoky ikithibitisha maamuzi yaliyochukuliwa na kuwa ushidi wa maazimio ya kikao hicho.

Ukweli ni kwamba TFF wamemaliza kiaina ili wasiwaumbue Simba waliokosea mkataba wao na wamewataka kufanya mazungumzo upya wakati ilitakiwa watangazwe kuchakachua mkataba.

Simba wanajua fika kwamba mkataba wa miaka miwili wa Singano ndio sahihi ndio maana wamekubali yaishe.

Endelea kufuatilia mtandao huu….tutakuletea Sinema nzima ya suala hili…
 
Ukiangalia utajua bwana mdogo hana akili nzuri, anapata ushauri mbaya au kuna mtu anamtumia. Kusema ana lala kwa kaka yake anapata salary ya 600,000 na posho pia na bado ana gari ya kazi ambayo hata ikimwingizia 10,000 kwa siku ni nying.halaf bado analala kwa kaka yake basi anaonesha bado ni mjinga.alikuwa na nafasi ya kuomba pesa ipande au kujipanga atoke vipi. Sijajua kwa sasa anaishi maisha gani na anapata tsh ngap.lakini je kwa umri wake mpira unaendeleaje?Je ameshafikia malengo?alipaswa kupata ushauri mzuri ataua kiwango chake cha mpira na kuna siku atatemwa huko aliko.kuna mwanamichezo anayeweza kutwambia huko aliko amecheza mech ngapi sasa na yukoje na yukoje uwanjan?

Shafii dauda ni wa kumuangalia sana, amechangia kumpoteza uyu dogo.
 
Katika hili inawezekana shafii dauda alikuwa na maslah sehemu au alitumika na sehemu moja katika hao wahusika? Kusema singano alikuwa analala kwa kaka yake huo ni upumbavu wa singano mwenyewe kama hajajipanga au pengine kaka yake alikuwa anamtumia? Sasa ni kumuuliza shafii dauda kipo wapi kilichompeleka singano azam? Anaendelea kufaidika na nini?

Shafii dauda ni wa kumuangalia sana, amechangia kumpoteza uyu dogo.
 
ALIPASWA KUJIFUNZA KWA AKINA NDEMLA, AJIB, MKUDE, ISIHAKA KUWA MVUMILIVU MPAKA AIVE SAWASAWA KISOKA. VILE VILE ALIPASWA ASINYEE KAMBI NA ANGEWEKA AKIBA YA MANENO. SIMBA NDIO TIMU PEKEE AMBAYO MCHEZAJI AKITAKIWA KWENYE MAJARIBIO NJE HUWA WANATOA RUHUSA HARAKA. HUKO ALIKO NAMUONEA HURUMA SANA ILA NUMUOMBEA KWA MUNGU AWEZE KUFANYA MAAMUZI YA BUSARA MBELENI KWANI KIPAJI KIKUBWA NAMANA ILE KINAOZEA BENCHI DAA INSIKITISHA.
 
Nilitokea kushangazwa Sana clouds kupitia kipindi Chao walishupalia Sana hili swala kilichonishangaza zaidi kuonyesha sehemu ambayo anaishi. Anyway ila MTU unapoondoka kwa mwajili na kwenda kwingine epuka kumsemea mabaya hata Kama kweli kulitokea kutokuelewana mfano mzuri Kama Uhuru selemani. Yaani like swala la singano lilichukuliwa Kama vile simba haikuwa na mchango wowote katika carrier ya jamaa nilishangazwa Sana. Ila aendelee kukomaa huko aliko anaweza kulidia kwenye Hali zaidi ya ile ya mwanzo.
 
Simba ndio timu pekee inayokuza na kulea vipaji vya vijana wadogo! Kijana mdogo akijituma vizuri simba atafurahia soka lake...
 
mimi kabla singano hajaenda azam niliwaza hivi timu ya azam ipo kibiashara zaidi staili ya mpira wa azam ni pasi tatu au nne goooooal sasa kijana singano ule mpira wa anakwenda anakwenda azam hawezi kucheza wadau waangalieni azam vizuri wanatumia nguvu nyingi katika kucheza mpira;mwangalie pasco wawa,chetche,himid mao,agre moris,mwantika,mugereneza hawa wote ni mpira ubaki mguu nenda
 
Katika hili inawezekana shafii dauda alikuwa na maslah sehemu au alitumika na sehemu moja katika hao wahusika? Kusema singano alikuwa analala kwa kaka yake huo ni upumbavu wa singano mwenyewe kama hajajipanga au pengine kaka yake alikuwa anamtumia? Sasa ni kumuuliza shafii dauda kipo wapi kilichompeleka singano azam? Anaendelea kufaidika na nini?

Shafii dauda ni wa kumuangalia sana, amechangia kumpoteza uyu dogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom