Ramadhani Kailima mkurugenzi wa uchaguzi wa Tanzania anahusikaje Zanzibar?

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
4,573
4,973
Tuliambiwa NEC haihusiku huko zanzibar,sasa huyu mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi fyokofyoko ya nini huko? alipaswa kukaa kimya ZEC wajiendeshe wenyewe maana hicho ni chombo huru.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Zanzibar.
 
Dhuluma.com wanahalalisha dhuluma! Hata Shein yuko radhi kupiga na kuua wapemba wenzake sababu ya chama......amekisaliti kisiwa sababu ya madaraka! Wapemba machozi yameenda na maji! Mtalia kwa nani awasikilize? USA au Jumuiya ya Kimataifa? CCM wako tayari nchi kuwekewa vikwazo vyovyote ila si Kuachia zbar iende CuF: Poleni sana wapemba na wapenda demokrasia wote! Udhalimu huu hadi lini????
 
Hawa Ndio wanaoichafua ZANZIBAR iwe kama wanavotaka, waone watu wanauana na kukiona kisiwa kinazama.
 
Kailima alienda kushuhudia uchaguzi wa mbunge wa jimbo ambao kimsingi upo chini ya NEC!
 
Acha ushamba wewe mbona hukuuliza jana Jaji lubuva akiongekea uchaguzi wa mbunge huko Zanzibar...Umemsusia mihogo nyani sasa unalia lia tu
 
Hawa Ndio wanaoichafua ZANZIBAR iwe kama wanavotaka, waone watu wanauana na kukiona kisiwa kinazama.

Jitahidi kujifunza kabla ya kukurupuka.

Kuna jimbo 1 la ubunge wa Jamhuri liliahirisha uchaguzu ambalo lipo chini ya NEC

Kailima kaenda kusimamia uchaguzi wa jimbo hilo na tayari mshindi amepatikana Shamsi Vuai Nahodha

Kitu kama hukijui usikurupuke ili mradi tu uonekane umeanzisha uzi huo ni uchonganishi na unafiki
 
Safi sana, MMEMFYATISHA MDOMO huyu mkurupukaji mpaka kakimbia!
Njoo huku weeee, Mpalakugenda, hamna kukimbia uzi!⛏⛏⚔⚰⚰⚰!
 
Tuliambiwa NEC haihusiku huko zanzibar,sasa huyu mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi fyokofyoko ya nini huko? alipaswa kukaa kimya ZEC wajiendeshe wenyewe maana hicho ni chombo huru.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Zanzibar.
nilichosikia ni kuwa huyo jamaa aliongelea ubunge wa kijitopele ambao mpaka sasa hivi nahodha wa ccm ameshinda wakati yule mshindani wake mkuu wa CUF hakushiriki.
Ubunge na urais wa jamhuri (bara na visiwani) upo chini ya nec ambayo mkurugenzi wake ni kailima.
ule wa wawakilishi, urais wa visiwani na masheha upo chini ya zec ambayo kailima hana mamlaka.
ila siungi mkono kwa serikali ya ccm inachokifanya zanzibar. maana ule ni ubakaji wa demokrasia.
 
Aiseee pole sana na ubakaji wa demokrasia. Ukizira wenzio wanakula. Mtu mzima unazira? halafu useme demokrasia imebakwa! hatari sana.
 
Tuliambiwa NEC haihusiku huko zanzibar,sasa huyu mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi fyokofyoko ya nini huko? alipaswa kukaa kimya ZEC wajiendeshe wenyewe maana hicho ni chombo huru.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Zanzibar.
Tafiti kabla ya kupost
 
Hawa Ndio wanaoichafua ZANZIBAR iwe kama wanavotaka, waone watu wanauana na kukiona kisiwa kinazama.
Kila siku mnalilia watu kuuana. Sijui mnaona raha gani kuua wenzenu kisa eti mnapiga uchaguzi au matokeo
 
Tuliambiwa NEC haihusiku huko zanzibar,sasa huyu mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi fyokofyoko ya nini huko? alipaswa kukaa kimya ZEC wajiendeshe wenyewe maana hicho ni chombo huru.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Zanzibar.
Mkuu huyo jamaa kazi yake ni maalum ambayo jecha aliifanya
 
Dhuluma.com wanahalalisha dhuluma! Hata Shein yuko radhi kupiga na kuua wapemba wenzake sababu ya chama......amekisaliti kisiwa sababu ya madaraka! Wapemba machozi yameenda na maji! Mtalia kwa nani awasikilize? USA au Jumuiya ya Kimataifa? CCM wako tayari nchi kuwekewa vikwazo vyovyote ila si Kuachia zbar iende CuF: Poleni sana wapemba na wapenda demokrasia wote! Udhalimu huu hadi lini????
Mkuu hakuna serikali dharimu iliyodumu milele hapa duniani,kama ilivyo kwa kiongozi dikteta hakuna aliyedumu milele na haya yoote tunayo yashuhudia kufanywa na ccm yana mwisho wake
 
nilichosikia ni kuwa huyo jamaa aliongelea ubunge wa kijitopele ambao mpaka sasa hivi nahodha wa ccm ameshinda wakati yule mshindani wake mkuu wa CUF hakushiriki.
Ubunge na urais wa jamhuri (bara na visiwani) upo chini ya nec ambayo mkurugenzi wake ni kailima.
ule wa wawakilishi, urais wa visiwani na masheha upo chini ya zec ambayo kailima hana mamlaka.
ila siungi mkono kwa serikali ya ccm inachokifanya zanzibar. maana ule ni ubakaji wa demokrasia.

Lakini aliongelea kuhusu UCHAGUZI wa Zanzibar na si wa Kijitokuwasha,sawa??
 
Tuliambiwa ZEC no Zanzibar Na NEC ni Jamhuri ya Tanzania lakini Jana Lubuva akazungumzia uchaguzi wa Zanzibar CCM bwana
 
Tuliambiwa NEC haihusiku huko zanzibar,sasa huyu mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi fyokofyoko ya nini huko? alipaswa kukaa kimya ZEC wajiendeshe wenyewe maana hicho ni chombo huru.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Zanzibar.
Kwani Zanzibar ni Kenya au?
 
Safari za nje zimefutwa isipokuwa kwa kibali cha rais na Sefue tu, ambaye alishatumbuliwa.
 
Back
Top Bottom