Raisi Magufuli kuwa kama Wazungu!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Jaribu kuwaiga Wazungu kwenye ufanyaji kazi kwao, wao huwa hawaangalii chozi la mtu bali hufwata sheria tu inavyotaka na hata kama ukilia chozi la damu kama umevunja sheria Mzungu atakuadhibu tu, na ndio maaana Wageni wanaokuwa deported na wazungu huwa wanalia machozi ya damu lkn Mzungu akisha simama Mlangoni kwako kwamba sasa unaondoka hakuna kitu utafanya hata ulie vipi atakubebea na kukuweka kwenye ndege, hivyo huyu mama Lwakatare chozi lake lisikufanye ulainike hiyo nyumba na nyinginezo ni lazima zibomolewe na haijalishi wenyewe watalia machozi ya aina gani, kama wangekuwa wazungu sasa hivi zamani hiyo nyumba imeshalipuliwa!!

Kumbuka Wazungu walivyojenga Reli na br. hapa nchini kuna watu wengi walikuwa wanagomea kufanya kazi lkn walikuwa wanakula viboko na kufanya kazi matokeo yake reli hiyo tunaitumia mpaka leo hii na ndiyo tegemeo letu kama Wazungu wangejali machozi ya babu zetu hizi reli zisingejengwa na hali yetu Kiuchumi ingekuwa mbaya zaidi, majumba hayo ya Kikoloni kama Makanisa na maofisi mpaka leo hii tunayatumia karibu ofisi zote za Serikali Mikoani zilijengwa na Wazungu!

Hivyo unavyofanya ni sahihi kabisa wengi watalia na kulalamika lkn hakuna maendeleo yasiyo na gharama na vizazi vijavyo kama vile leo hii tunavyoringia reli na majumba mazuri ya kikoloni pia watoto wetu wataringia nchi nzuri iliyotunza mazingira, fukwe zake zote zikiwa wazi kwao kuzitumia kwa jinsi wanavyopenda, na wewe pekee ndiyo mwenye makende ya kufanya hilo kama wewe ukishindwa basi hii nchi tutaipoteza na haitarudi tena!
 
Mimi nijuavyo ili ufanye vitu kama mzungu ni aidha uwe umesoma kwao au uliwahi kufanya nao kazi hivi mkuu wetu wa kaya ana exposure ya kutosha na hawa jamaaa?
 
Mimi nijuavyo ili ufanye vitu kama mzungu ni aidha uwe umesoma kwao au uliwahi kufanya nao kazi hivi mkuu wetu wa kaya ana exposure ya kutosha na hawa jamaaa?

Hata huyu aliyeleta mada hana exposure kabisa , hajui kwamba wazungu hawawezi tesa raia zao ndani ya nchi yao , bila solution mbadala ,angalia ubomoaji wa huko mambondeni unavyo athiri wanawake watoto,wagonjwa na wazee .
 
Waliojenga mabondeni wote walipewa Viwanja vya bure kabisa Mabwepande na fidia juu pmj na mifuko ya cement na mabati ya kuanzia lkn waliviuza viwanja na kurudi Mabondeni sasa ulitaka Serikali ifanye nini tena zaidi ya hapo?
Hata leo hii wakitaka viwanja Mabwepande wanapewa bure kabisa lkn hawataki wanataka kubakia mjini na kuishi kwenye mitaro, Seriklai ifanyeje? Embu toa ushauri!
 
Bado huja tambua wazungu wangwezaje handle hili suala , ndio maana na sema huna exposure kabisa.
 
Bado huja tambua wazungu wangwezaje handle hili suala , ndio maana na sema huna exposure kabisa.

Sijui kama uliona zile video za watoto wakilia, pale tuu kama ungekua na exposure hata kidogo ya kutambua wazungu wana handle vipi masula kama hayo ungetambua kabisa namna ya ku deal na suala hilo, ila umeshindwa , wazungu hawa kurupuki wanaplan nzuri na endelevu na inayo protect wasio jiweza, hii ingekua kwa wazungu teari watu wangejidhuru ni kashfa kubwa .
 
Hata huyu aliyeleta mada hana exposure kabisa , hajui kwamba wazungu hawawezi tesa raia zao ndani ya nchi yao , bila solution mbadala ,angalia ubomoaji wa huko mambondeni unavyo athiri wanawake watoto,wagonjwa na wazee .
Kwani majanga ya mafuriko maeneo hayo wanayobomolewa si zaidi ya kubomolewa????!!!. Kubomolewa unaweza ukaokoa baadhi ya mali zako iwapo utakuwa mtiifu kwa notisi unayopewa. Kubomolewa hakuwezi kupelekea watu kupoteza mafuriko. Mafuriko ya jangwani mwaka juzi yaliua watu watatu na watoto wanne walipotea.
 
Bado huja tambua wazungu wangwezaje handle hili suala , ndio maana na sema huna exposure kabisa.

Wazungu hawawezi kukubali mtu avunje sheria na wakamuachia hata siku moja kwanza siyo Wazungu tu bali watu wote walioendelea kama Wajapani, Wasingapore, Korea n.k
 
Wazungu hawawezi kukubali mtu avunje sheria na wakamuachia hata siku moja kwanza siyo Wazungu tu bali watu wote walioendelea kama Wajapani, Wasingapore, Korea n.k
Ndio maana na sema bado huan exposure, wani ungesha tambua hii ishu inge kua handle kwa namna gani , kwamaana hata ingekua imetokea kama una wajua wadhungu wanavyothamini wananchi wao, wasinge weza fanya serikali ilicho kifanya , mipango na mikakati ingekua bora zaidi kutekeleza hali iliyo jitokeza
 
Acha kudanganya hapa, Marekani watu wasiokuwa na Makazi ( homeless) ni zaidi ya milioni tatu yaani hawa ni watu wanaolala kwenye mitaro , chini ya madaraja na wengine barabarani na hii ni pamoja na watoto wadogo, wakati hapa kwetu watu waliovunja sheria za nchi wamepewa viwanja bure kabisa bila kulipia hata shilingi pmj na mifuko ya cement lkn wameviuza jambo ambalo kama ingekuwa nchi za Wazungu hawa watu wangefunguliwa mashitaka kwa maana ya udanganyifu wameuza mali waliopewa bure na Serikali!
 
Wewe uwenda huna hata banda la kuku na ndio maana umeamua kuropoka tuu kama mtu hasiye na uwezo wa kutakali mambo,
 
Kuvunjiwa ni rahisi kushabikia kama siyo mhanga wa hiyo bomoa bomoa au hata haujaona jinsi watoto wanavyopata shida kutokana na kutokuwa na kivuli cha kupumzika wala kulala.
Hebu jaribu kuvaa kiatu chao chapo kwa sekunde tu.
Serikali naomba iwasaidie hawa watu japo kweli walifanya makosa kwa kuivunja sheria kujenga na kuishi kusipofaa.
INAPENDEZA SANA MTU ANAPOPEWA ADHABU YA KUMFUNDISHA NA SIYO KUPEWA ADHABU YA KUMFANYA AWE KATILI ZAIDI AMA AENDELEE KUFANYA MAKOSA ZAIDI.
 
Mimi nijuavyo ili ufanye vitu kama mzungu ni aidha uwe umesoma kwao au uliwahi kufanya nao kazi hivi mkuu wetu wa kaya ana exposure ya kutosha na hawa jamaaa?
Kwa mentality kama yako basi hao wazungu wana kila sababu ya kukurushia ndizi mbivu
 
Kwa mentality kama yako basi hao wazungu wana kila sababu ya kukurushia ndizi mbivu
Wewe pongo hiyo keyboard au hako kasimu unakatomia kenyewe ndio wamekuwezesha nini ambacho tuliwahi anzisha sisi?
 
Wazungu hawawezi kukubali mtu avunje sheria na wakamuachia hata siku moja kwanza siyo Wazungu tu bali watu wote walioendelea kama Wajapani, Wasingapore, Korea n.k

Wazungu wasingekupa nafasi ya kuvunja sheria kwa sababu wangebandika matangazo kama sehemu hii hairuhusiwi kujenga na halmashauri wangekuzuwia unapoanza kufyeka tu.
 
Haitaji kufanya kazi kama mzungu au exposure kuona sheria. Kuna viongozi wengi walisoma nnje, wangine wamesafiri sana(JK) lakini wameshindwa kufanya kazi zao kama wazungu.
 
Bado huja tambua wazungu wangwezaje handle hili suala , ndio maana na sema huna exposure kabisa.

CamaDume,
Uko sahihi mwanakwetu.Kuna mijitu ndani ya nchi hii kazi ni kushabikia kila kitu hata kama ni cha kipuuzi.Mijitu hii mara nyingi ni ya CCM.Mijitu ya Copy&Paste!

Magufuli na serikali lazima wakumbuke kuwa kwa sasa kuna kitu kinaitwa MABADILIKO YA HALI YA HEWA kwa kimombo GLOBE WARMING.Tatizo hili liko dunia nzima hata huko Marekani na Uchina tunaona nchi hizo kubwa na zenye Uchumi imara zikikumbwa na mafuriko kila mwaka lakini hatujaona Ma-bulldozer yakivamia na kuvunja nyumba za wananchi wanaokumbwa na mafuriko!

Kinachofanywa na serikali ya CCM ni uonevu na uvunjaji wa haki za binadamu.Sheria zinasema haki za msingi za binadamu ni Chakula na MALAZI/HIFADHI kwa kimombo SHELTER/HOUSING! Lakini cha ajabu CCM wanavunja nyumba za Wananchi wake kwa kisingizio cha mafuriko!Kwa maana hiyo wewe ukishapitiwa na mafuriko ni kosa! Hakuna cha kulipwa wala kutafutiwa eneo au hifadhi mbadala. HUU NI UKABURU uliopitiliza!

Onyo kwa CCM, endeleeni kuvunja tu kwa sasa mmeshika mpini. Kumbukeni mwaka 2020 siyo mbali kwani bado miaka 4 tu imebaki.Tutakutana kwenye sanduku la Kura nataka niwaambie hali yenu itakuwa mbaya zaidi kuliko ilibyokuwa 2015. Tusubiri!
 
Mkuu Barbarosa si lazima raisi afanye kama hao wazungu kwani mbona tokea aaapishwe anafanya hayo?

1. Anabana matumizi ili serikali ipate fedha za kujiendesha. Hii inafanywa sana huko kwa wazungu kwani kuna kodi za maendeleo na tozo zingine tu ambazo ni lazima tu mtu atalipa la sivyo sharia itatafsiriwa kwa vitendo.

2. Anatafsiri sheria zilizopo (tena ziko kichwani hasa sheria za ardhi) kwa vitendo kupitia watendaji wake ambao ni mawaziri na makatibu wakuu na wengine.

3. Ametengeneza kitu kinaitwa KPI (Key Performance Indicators) ambapo watendaji wake wote ni lazima wakifike viwango vya utendaji unaoridhisha la sivyo wataachia ngazi na wamesaini mikataba.

Hayo mambo yote yanafanyika Ulaya na nchi zingine zinazofuata sheria.

Hivyo bila hata kuwa na "exposure" ya huko Ulaya kwa wala mayai, yeye raisi JPM anafanya mambo hayohayo ya wazungu unayotaka akiwa hukuhuku Afrika.

Halafu kuna kundi fulani la watu wazito ambao wameanza kufanya kampeni za chinichini za kukwamisha jitihada za serikali hii ya JPM.

Pia vyombo vya habari havina budi kuwa makini na aina ya vichwa vya habari ambavyo vinalenga kuoanisha juhudi hizo za watu hao.

Kwa mfano leo hii gazeti la Mwananchi la mtandaoni lilikuwa limeweka kichwa cha habari kinachosema kwamba "mchungaji Rwakatare amvimbia raisi JPM", lakini baada ya kutafakari kichwa hicho cha habari na madhara yake mhariri wa gazeti hilo akaamua kubadili kichwa hicho haraka ilivyowezekana na kuweka kichwa kinachosema "Mchungaji Rwakatare aivimbia serikali".

Ujumbe wa kichwa hicho unaweza kuwa tofauti kabisa na yaloelezwa katika taarifa hiyo kwamba ni watakelezaji wa amri ya Wizara ya Ardhi ya kubomoa nyumba iliojengwa kwenye hifadhi ya mikoko walikwenda kuweka alama ya X kuashiria ujio wa bomoabomoa katika eneo hilo na sio raisi JPM.
 
CamaDume,
Uko sahihi mwanakwetu.Kuna mijitu ndani ya nchi hii kazi ni kushabikia kila kitu hata kama ni cha kipuuzi.Mijitu hii mara nyingi ni ya CCM.Mijitu ya Copy&Paste!

Magufuli na serikali lazima wakumbuke kuwa kwa sasa kuna kitu kinaitwa MABADILIKO YA HALI YA HEWA kwa kimombo GLOBE WARMING.Tatizo hili liko dunia nzima hata huko Marekani na Uchina tunaona nchi hizo kubwa na zenye Uchumi imara zikikumbwa na mafuriko kila mwaka lakini hatujaona Ma-bulldozer yakivamia na kuvunja nyumba za wananchi wanaokumbwa na mafuriko!

Kinachofanywa na serikali ya CCM ni uonevu na uvunjaji wa haki za binadamu.Sheria zinasema haki za msingi za binadamu ni Chakula na MALAZI/HIFADHI kwa kimombo SHELTER/HOUSING! Lakini cha ajabu CCM wanavunja nyumba za Wananchi wake kwa kisingizio cha mafuriko!Kwa maana hiyo wewe ukishapitiwa na mafuriko ni kosa! Hakuna cha kulipwa wala kutafutiwa eneo au hifadhi mbadala. HUU NI UKABURU uliopitiliza!

Onyo kwa CCM, endeleeni kuvunja tu kwa sasa mmeshika mpini. Kumbukeni mwaka 2020 siyo mbali kwani bado miaka 4 tu imebaki.Tutakutana kwenye sanduku la Kura nataka niwaambie hali yenu itakuwa mbaya zaidi kuliko ilibyokuwa 2015. Tusubiri!

MKuu, kwani ni lini hawa wananchi wenzetu walianza kuambiwa wahame?
 
Back
Top Bottom