DAWASCO kateni maji hata kama ni Ikulu..Haya ni maneno yalisemwa na raisi wetu JPM, natumaini
DAWASCO hawatakuwa na visingizio tena kwamba watu hawalipi bills zao tena, JPM anajuwa alisemalo, kwenye bajeti, Idra, Taasisi, Mashirika na Wizara zote huwa zinatengewa bajeti ya maji, haoni sababu kwanini hawalipi na kaamuru na kuwapa meno
DAWASCO kukata maji na kukusanya hayo malipo...
JPM kaenda mbali zaidi na kutaka CEO wa
DAWASCO Mutalemwa (a true dinosaur) kuachia ngazi, huyu ndiye alikuwa kinara wa uozo wote pale, kutokana na hii kata maji, ma DC, ma RC na ma DED watapigwa chini wote (Gazeti la Mtanzania).
Hongera JPM, sasa twaongea lugha moja...