Rais Magufuli awaapisha kiapo cha uadilifu Makamishina/Manaibu waliopandishwa vyeo Ikulu

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386


Magufuli nadhani yupo na wale maaskari aliowapandisha vyeo..

=> Kawapa Rungu kawaambia yale mambo ya unanijua mimi nani... Hakuna...
Na kawaambia kuwa polisi wafanye kazi zao..

=> Kuhusu meli kupungua bandarini kasema bora zisije kama hazilipi kodi.

=> kuhusu watalii kasema bora awe na watalii laki tano wanaolipa kodi kuliko watalii mia mbili ambao hawalipi kodi.

=> kasema raia wote ambao wanafanya kazi kwenye jeshi la Polisi waondolewe wote kuanzia kwenye uhasibu na kazi zingine waondolewe warudishwe utumishi..

=> kasema kaambiwa kuwa Sinza nyumba zimekosa watu.. Kacheka anadai watu walikuwa na kufuru.. Mtu mmoja anapangishia michepuko mitatu minne... Na week end anaenda Dubai na kurudi..

=> Polisi wakikamata gari hata kama ni ya RPC waachwe na sheria ifuate mkondo wake. Katolea baadhi ya mifano ya magari kama Happy Nation alisikia kuwa haya magari na mengine ukiyakamata bara barani ujue utahamishwa na kituo..

Leo Rais JPM alikuwa Ikulu akiwaapisha Manaibu Kamishna wa Polisi(DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi(SACP) wapatao 58 kati ya 60 waliopandishwa vyeo hivi karibuni.
Katika mambo yote Rais amegusia suala la maslahi kwa jeshi la polisi,rushwa na nidhamu katika utumishi.

Akiongelea Rushwa,Rais JPM anasema Jeshi la Polisi lijiepushe sana na vitendo vya rushwa vinavyolikosesha heshima katika jamii,anasema hivi karibuni amepata taarifa za rushwa kubwa ndani ya jeshi la polisi inayokadiliwa kuwa kati ya bilioni 40 hadi bilioni 60 ambazo zilipaswa kununua sare za jeshi la polisi lakini hakuna hata sare moja iliyonunuliwa,na wakati huohuo kuna magari karibu 70 ya jeshi la polisi yapo bandarini na hayakakombolewa,hivyo katoa maagizo uchunguzi wa haraka ufanyike na sehemu ya pesa hiyo ikalipie magari hayo haraka na yatoke bandarini.

Rais pia ameagiza jeshi la Polisi kuondoa utaratibu wa kuwaondoa Raia wote ambao ni watumishi wa jeshi la polisi na kuweka nafasi hizo kwa Polisi walio na taaluma hiyo,na kama hawana wataalamu basi waajiri watu ambao ni wataalamu wa fani hizo ambao watakuwa ni Polisi ndani ya jeshi na si raia,Anasema inashangaza moja ya wizi uliogundulika ni wa muhasibu mkuu wa Polisi ambaye ana tuhuma za ubadhirifu wakati ni raia ndani ya Jeshi,kiasi kwamba Polisi wanakimbizana na wezi wa kuku mtaani wanaacha wezi wa mabilioni walio ndani ya makao makuu ya Jeshi la Tanzania.

JPM pia anasema hakuna umuhimu wa kitu kinaitwa Polisi Jamii,anasema huwezi kuwa polisi ndani ya Maji ziwani unamkamata jambazi anateka wavuvi halafu unaanza kujadiliana nae wakati una bunduki na pisto,"Unajadiliana nini na jambazi?" Alihoji Rais JPM...dawa ya huyo ni kumlaza tu chini,huwezi kuwa Polisi halafu unachekacheka na muhalifu na huku una bunduki mkononi.Rais anasema hizo bunduki wanapewa kwa ajili ya kuzitumia,maana inafikia polisi hadi anapokwa silaha na jambazi kisa polisi jamii.Rais anasema inatakiwa ifike sehemu mtu akimuona Polisi aanze kuogopa,hayo mambo ya Polisi jamii ndio yanaongeza uhalifu,hakuna urafiki wa Polisi na Raia

Rais anasema kuna wakati watu walivamia kituo cha Polisi Chato,wakachoma moto na kuiba silaha,halafu mkuu wa kituo ana bastora kiunoni na bunduki,anabaki kusema "Polisi Jamii",hakuna kitu kama hicho,wale watu wote waliokuja kuchoma kituo ilibidi "walazwe chini".Hata kama yeye akikutwa ndugu yake "amelazwa chini" kwa tukio kama hilo basi atawapongeza polisi,maana hiyo ndio kazi yao na lazima kuwe na heshima kati ya polisi na raia.Wakuu wa Polisi wasiwasumbue askari wa chini wanapotumia nafasi zao "kuwalaza watu chini" hasa pale wanapokuwa wanaliletea mchezo jeshi la Polisi.

Ameviomba vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kukaa pamoja na kushirikiana,ameagiza Polisi kuendelea kumsaidia kukusanya mapato kwa kuongeza ulinzi bandarini,kwani ni baora akawa na makontena machache yenye kulipa kodi kuliko kuwa na lundo lisilolipa kodi.

Rais anasema huko Sinza amepewa taarifa nyumba zinabaki tupu na watu wanakimbia,anasema na bado...maana watu walizoea kupangia "michepuko" upande mzima,unakuta mtu ana "michepuko" mitatu au zaidi na kila mmoja kampangia upande,weekend anaenda Dubai kwa shopping,hizo zote zilikuwa hela za wizi wizi.Sasa hakuna pesa ya bure,lazima watu wafanye kazi.

Mwisho Rais kawaasa polisi kuepuka kupendeleana,hata kama gari la RPC limevunja sheria za barabaranu ni kulikamata na kuchukua hatua.Akachombeza kidogo "Unakuta traffic police anapewa shilingi 5000 njiani ya kubrash viatu kwa kushinda juani na kwenye mvua watu wanasema rushwa,wakati kuna watu wanaiba mabilioni ya pesa.

Wadau amani iwe kwenu.

Katika kuhakikisha kuwa kunakuwa hakuna mwingiliano wa majukumu baina ya Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Utumishi wa Umma, Rais Magufuli leo aamemwagiza IGP kuorodhesha majina ya watumishi wote ambao si Polisi na ayapeleke Utumishi wa Umma ambako watapangiwa majukumu mengine. Hayo ameyasema leo Ikulu Jijini Dar es Salaam aliposhuhudia kiapo cha Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi. Amesema jeshi ni jeshi na raia ni raia. Kunapokuwa na muingiliano baina ya jeshi na Raia kunatengeneza mwanya wa ubadhilifu.

Ametolea mfano wa Frank Charles Msaki, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa jeshi la Polisi ambaye alikuwa anawalipa posho ya chakula watumishi ambao si polisi hali iliyopelekea upotevu wa zaidi ya milioni 300. Amesema kuwa Msaki alikuwa jeuri na alikuwa na mamlaka ya kumfokea hata askari ijapokuwa yeye si Askari kwa vile tu alikuwa anashika fedha.

Aidha, Rais anasema kuwa mchanganyiko huu ulisababisha jeshi la polisi kushindwa kuwachukulia hatua za kinidhamu Raia wanaofanya kazi kwenye jeshi lao kwa vile misingi ya kuchukuliana hatua baina ya polisi na Utumishi wa Umma ni tofauti.

Ijapokuwa kauli hiyo ameitoa kwenye hafla ya kula kiapo kwa Makamishna Wazaidizi wa Jeshi la Polisi, ameagiza pia vyombo vyote vya Dola kutekeleza agizo hilo kwa vile viongozi wa vyombo vyote vya dola walihudhuria hafla hiyo.
 

Attachments

  • 13726734_1124334634312462_33600281238670896_n.jpg
    13726734_1124334634312462_33600281238670896_n.jpg
    16.2 KB · Views: 124
Akizungumza Ikulu na maofisa wa Polisi walio pandishwa vyeo Leo, Rais ameshangaa Traffic wanaopata shida ya kunyeshewa mvua barabarani eti wakipewa 5,000 ya kubrashi viatu watu wanaita rushwa wakati kuna watu serikalini wanaiba mafedha?
Hiyo ni kauli ya Rais wetu.
Source; TBC 1
 
(Nimeisikiliza hotuba.. Kuhusu elfu tano naona watu wanaanza kumquote rais vibaya..na hili ndio tatizo la watanzania.. Msimquote vibaya Rais hajahalalisha rushwa.. Ila ni kama alikuwa analalamika na kuwapa sifa polisi kuwa ni waadilifu akasema huko Serikalini kuna watu walikuwa wanaiba mamilioni ila hawasemwi na wanapeta lakini Polisi walikuwa wanasema kwa kuchukua elfu tano tu.. Ni kama alikuwa anawaambia kuwa sasa hivi haluna cha mkubwa.. Wote heshima..(dont quote wrong Rais wetu mimi nimemsikiliza mwanzo mwisho)


Nashukuru kwa kutoa tahadhari kwa wale wazito wa kufikiri.. Na wapotoshaji
 
Sasa huyu wa dar akisikia hivyo na yeye anajiona Raisi wa dar, kesho utasikia mashoga wote wajisalimishe, wasio na kazi wajisalimishe, wavuta shisha na sigara hadharani wajisalimishe, machangudoa wajisalimishe, badala ya kushirikiana na viongozi wengine wa kisiasa waliochaguliwa na wananchi na kujenga mahusiano mazuri ili kuwaletea wananchi maendeleo anakomalia matamko yasiyo ya msingi.
Matatizo ya msingi ya wana dar ni haya hapa:-
1. Maji safi na salama,
2. Majitaka na uchafu
3. Barabara mbovu
4. Upungufu wa madarasa, madawati, na vitendea kazi vingine mashuleni
5. Sehemu za kufanyia biashara machinga
6. Uhalifu wa aina mbalimbali pamoja na ujambazi
 
Wadau amani iwe kwenu.

Katika kuhakikisha kuwa kunakuwa hakuna mwingiliano wa majukumu baina ya Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Utumishi wa Umma, Rais Magufuli leo aamemwagiza IGP kuorodhesha majina ya watumishi wote ambao si Polisi na ayapeleke Utumishi wa Umma ambako watapangiwa majukumu mengine. Hayo ameyasema leo Ikulu Jijini Dar es Salaam aliposhuhudia kiapo cha Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi. Amesema jeshi ni jeshi na raia ni raia. Kunapokuwa na muingiliano baina ya jeshi na Raia kunatengeneza mwanya wa ubadhilifu.

Ametolea mfano wa Frank Charles Msaki, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa jeshi la Polisi ambaye alikuwa anawalipa posho ya chakula watumishi ambao si polisi hali iliyopelekea upotevu wa zaidi ya milioni 300. Amesema kuwa Msaki alikuwa jeuri na alikuwa na mamlaka ya kumfokea hata askari ijapokuwa yeye si Askari kwa vile tu alikuwa anashika fedha.

Aidha, Rais anasema kuwa mchanganyiko huu ulisababisha jeshi la polisi kushindwa kuwachukulia hatua za kinidhamu Raia wanaofanya kazi kwenye jeshi lao kwa vile misingi ya kuchukuliana hatua baina ya polisi na Utumishi wa Umma ni tofauti.

Ijapokuwa kauli hiyo ameitoa kwenye hafla ya kula kiapo kwa Makamishna Wazaidizi wa Jeshi la Polisi, ameagiza pia vyombo vyote vya Dola kutekeleza agizo hilo kwa vile viongozi wa vyombo vyote vya dola walihudhuria hafla hiyo.
 
Back
Top Bottom