Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Nianze kwa kumpongeza Raisi kwa kuonyesha dhahiri aina ya uongozi ambao zimepita siku nyingi hatujashuhudia hasa kwa vijana wengi ambao wamezaliwa miaka ya 80 na 90.
Aina ya uongozi na mbinu zako ndizo haswa zinahitajika kwa hali ya nchi ilipofika..nchi haikuwa na "chain of command"..maagizo kutoka juu hayakutekelezwa kiasi kwamba kila mtu alikuwa "kambale". Kuna mambo nayaainisha ambayo ni matokeo ya uongozi wako.
1.Viongozi wateule wako sasa wanawajibika na maagizo yao yanatekelezwa kwa kiwango kikubwa.
2.Mtindo wako wa kueleza hadharani sababu za kutengua teuzi ni mzuri kwani wengi wameingizia serikali/wananchi hasara,waliiba hadharani huku wananchi wakikosa huduma hivyo ni stahiki yao pia tuwazomee...na hapa naweka wazi watu hawa walitajwa na ripoti za CAG na hata wananchi tulitowa tuhuma zao ila walikuwa "kambale".
3.Umendoa mtindo wa chunguzi juu ya chunguzi...ambao leo kuna malofa kwa kivuli cha "watetezi wa haki za binadamu"...wanajaribu kupata umaarufu wa kupinga kila jambo bila mafanikio.
3.Nimefurahi kuwa kila mara umetambua tuliokupa ajira ni sisi wananchi na sio wabunge au wanasiasa uchwara...na magenge ya oya mafisadi.
4.Umeitenganisha familia yako na ikulu hili nakusihi ulisimamie kwani ulifanya tokea kwenye kampeni hadi genge la mafisadi likaeneza propaganda chafu dhidi yako...kwani upande wao mama na watoto ndio walikuwa wanashika koba la hela wakizunguka huku na kule kuhadaa wapiga kura.
6.Umeonyesha tofauti kwa kuondoa matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza pesa hizo zije kutoa huduma kwa wananchi,hili jambo limetuonyesha wanasiasa wanafki wasio na huruma na wananchi wakilalamika eti "nani kakupa kibali?",kwao tisheti,maji,kwenda kuangalia nyumba za balozi ni bora kuliko madawati na barabara!
7.Mtindo wako wa usimamizi wa fedha umewaumbua wakuu wa mashirika ya umma kuwa wana wajibu wa kuchangia mfuko wa hazina na sio kugawana ziada kwa marupuru na bonasi za ujanja ujanja ili mradi tu kupunguza ziada/faida na ninaunga mkono uamuzi wako wa kuweka "ceiling" ya mishahara huku kila mwaka mashirika hayo yakipata ruzuku na nyongeza ya mtaji kutoka hazina.
8.Kutokuwa na madalali hapo magogoni kumewaumbua sana hata wazungu ambao hutumia makuwadi wao kutengeneza namna ya kuingia mikataba feki.
Ninakusihi udumishe huo mtindo wako ili adabu iwepo,ninakushauri kwa wafanyakazi vyeo vya wakurugenzi waajiriwe kwa mikataba ili kuepuka kuwaweka serikalini muda mrefu aina ya Wilson Kabwe..ambaye ana mkataba wa kudumu huku wakituumiza.Hii husaidia pia kuongeza nidhamu katika kazi...,ajira za kudumu zimeleta nidhamu na uawajibikaji kwa wakurugenzi wa mashirika ya umma ifike muda wakurugenzi wizarani na halmashauri wasiwe na mikataba ya ajira za kudumu
Nawasilisha,karibuni kwa hoja