Rais wetu Samia amekuwa kielelezo bora

Rais wetu Samia amekuwa kielelezo bora

Mukua

Senior Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
157
Reaction score
203
Kwa kazi alizozifanya kwa kipindi kifupi hiki kwenye uongozi wake umedhihirisha wazi kuwa ni kiongozi mwenye kipawa Cha hali ya juu Sana, hekima, uchaji Mungu, upendo,, vyote na vingine vingi vimesheheni katika maisha yake ya uongozi.

Kwa hili la kuwaunganisha watanzania na kuonyesha wazi kuwa kwenye siasa hakuna uadui bali ni kushindana kwa hoja halipaswi kupita bila ya kupongezwa.

Japo niwazi kabisa kuwa wapo waliopigwa upofu wa ubinafsi na chuki , yaani ambao hata mema yakifanyika kwao hao hawaoni, watu Kama hao ni kuwasamehe kwani hawajui watendalo Ila iko siku watakiri kuwa wewe ni Rais Bora aliyepata kuwepo kwenye taifa letu.

Tanzania ni yetu sote waruhusu wapinzani waseme bila ya kuvunja Sheria , waonyeshe wapi Mambo hayaendi sawa Kama ni kweli ili iwe rahisi kwako kurekebisha na taifa letu lisongele mbele.

Siku zote mtu aliye Makini ni yule anaye pokea mawazo mbadala toka kwa watu tofauti tofauti Kisha huya chakata na kufanyia kazi Yale yaliyo mazuri.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu na kazi iendelee.
 
Anajitahidi ila anapaswa kuwa makini na Chawa wa Mama na Genge S, hawa watamwangusha
 
Binafsi naona iwekwe kwenye katiba Marais JMT wawe wanawake na watoke Zenji, maana wakitoka bara inaweza kutokea Covid-19, hawaaminiki!
 
Anajitahidi ila anapaswa kuwa makini na Chawa wa Mama na Genge S, hawa watamwangusha
Ni kweli Kila analotenda linaonekana kwenye dhamiira yake. Hasa upendo alionao kwa anao waongoza.
 
Back
Top Bottom