Rais wetu, focus yako iwe vitendo

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
Rais wetu anaongea sana kuliko vitendo, na anaongea mambo yaleyale wakati hali mitaani inazidi kuwa ngumu. Tunataka kuona viwanda, ajira, mishahara imara kwa wafanyakazi, mipango ya kilimo cha umwagiliaji, pembejeo kwa wakulima, mikopo ya elimu ya juu kwa vijana wote, bima za afya kwa watanzania, LUGUMI wanakamatwa, fedha za waathirika wa tetemeko zinarejeshwa n.k.
 
Ila kiukweli mjomba anaongea sana, nadhan anaongea kuliko MTU yoyote aisee,
Alafu mr mkiki umegusa pazuri, swala lakuwasumbua wastaafu inaumiza sana. Kweli wastaafu niwakukalishwa halmashauri eti uwahakiki ndio wapewe chao.
 
Rais wetu anaongea sana kuliko vitendo, na anaongea mambo yaleyale wakati hali mitaani inazidi kuwa ngumu. Tunataka kuona viwanda, ajira, mishahara imara kwa wafanyakazi, mipango ya kilimo cha umwagiliaji, pembejeo kwa wakulima, mikopo ya elimu ya juu kwa vijana wote, bima za afya kwa watanzania, LUGUMI wanakamatwa, fedha za waathirika wa tetemeko zinarejeshwa n.k.

Pole sana. Aliyekwambia anayekuletea maendeleo ni nani? Fanya kazi acha kulalamika! Fedha iliyoadimika mitaani ni yako? Ninyi ndio mnaokanganya watu. Fedha hakuna mtaani - fedha hakuna mtaani, kuna mtu amechukua fedha kwenye akaunti yako bila ridhaa yako? Kama ni mtumishi, hulipwi mshahara wako? Kama ni mfanya biashara, kuna aliyezuia wateja wasije kwako kununua bidhaa? Mbona kila kitu Magufuli Magufuli?

Vitendo vipi unavyotaka kuviona? Hujaona barabara ya mwenge morocco? Hujaona kazi inayofanyika pale tazara junction? Hujaona shirika la ndege likihuishwa? Hujaona kutimuliwa majipu yakifumuka kama vifuu? Hujaona kinachoendelea ujenzi wa reli?

Sio lazima kila kitu amalize leo? Lakini acha kulalamika, fanya kazi upate mshahara wako. Unaomba kuongezewa mshahara kwa kipi cha ziada ulichofanya? Ni kuomba kuongezewa tu!! Fanya kazi!
 
Bhado yupo kwenye kampeni
 
Kosa kubwa.ni kuamini maendeleo ya nchi na watu wake yataletwa na wananchi.kama marekani isingekuwa na viongozi imara Leo hii isingekuwa,China,urusi,south Africa n.k.uongozi bora ndo chanzo cha maendeleo.utajiri uliokuwepo Tanzania. Tunaweza tukaishi kama Libya ya Gaddafi.lakini hatujapata kiongozi bora.wa kusimamia maliasili zetu.
 
Umesema vizuri. Wajibu wako mwananchi ni upi katika kuleta maendeleo? Unajua utamaduni wa watu walio nchi zilizoendelea hasa katika viwanda na technology? Unajua wajapan wanalala masaa mangapi? Kiongozi anaonyesha njia lakini maendeleo yanaletwa na watu kwa kufanya kazi.

Sisi kwa kiasi kikubwa ni wavivu na wanaotega sana kufanya kazi. Ni kulalamika tu muda wote lakini kazi tunafanya? Maofisini watu wanawaza deals tu na safari ma semina. Ni pesa tu! Sawa, pesa, lakini kazi inafanyika?

Nchi hizo zimeendelea, unajua utamaduni wao katika kulipa kodi? Hapa mtu akiweka kodi basi kelele mpaka basi. Maendeleo sio kitu rahisi rafiki, tufanye kazi!
 
Nikipata elimu bora,ajira,au kujengewa uwezo wa kujiajiri,afya bora,miundombinu bora,mitaji ya kufanyia biashara n.k.Leo hii waulize serikali ni vijana wangapi hawana ajira wapo tu mitaani haijui.maendeleo yanaanza na uongozi bora.sisi tutafuata.
 
Pole sana. Aliyekwambia anayekuletea maendeleo ni nani? Fanya kazi acha kulalamika! Fedha iliyoadimika mitaani ni yako? Ninyi ndio mnaokanganya watu. Fedha hakuna mtaani - fedha hakuna mtaani, kuna mtu amechukua fedha kwenye akaunti yako bila ridhaa yako? Kama ni mtumishi, hulipwi mshahara wako? Kama ni mfanya biashara, kuna aliyezuia wateja wasije kwako kununua bidhaa? Mbona kila kitu Magufuli Magufuli?

Vitendo vipi unavyotaka kuviona? Hujaona barabara ya mwenge morocco? Hujaona kazi inayofanyika pale tazara junction? Hujaona shirika la ndege likihuishwa? Hujaona kutimuliwa majipu yakifumuka kama vifuu? Hujaona kinachoendelea ujenzi wa reli?

Sio lazima kila kitu amalize leo? Lakini acha kulalamika, fanya kazi upate mshahara wako. Unaomba kuongezewa mshahara kwa kipi cha ziada ulichofanya? Ni kuomba kuongezewa tu!! Fanya kazi!
Nimejifunza kutoka mazingira ya sasa kwamba, tunaweza kuweka mdudu yeyote pale ikulu, awe inzi, mbu, mbung'o, kunguni au chawa, tukampa vyeo vikuu vitatu, amiri jeshi Mkuu, Mkuu wa nchi na mkuu wa serikali. Na watu watamuheshimu, jeshi litamtii, na serikali yake itaogopwa. Kwa namna mambo yanavyoenda sasa hivi, hatuna tofauti na wadudu.
 
Back
Top Bottom