Rais wangu unajiskiaje?

Rais wangu unajiskiaje?

GNA

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
246
Reaction score
72
Rais wangu unajiskiaje unapokaa Ikulu hauumwi maleria, lakini sisi wananchi wako huku kwa Mtogole maleria ni vitu tulivyo zoea, una jiskiaje unachotaka kula unakula lakini wananchi wako kinacho patikana ndio wanakula. Unajiskiaje mtoto wako anaweza kusoma hadi chuo either amepata mkopo au la, unajiskiaje wamama wajawazito,wanavyo lala kwenye vitanda wawiliwawili, huko Amana,Tmk, wakati mkeo, hapitii huko, nauliza unajiskiaje,? Unajiskiaje watu wanapohoji Twiga wamepandaje ndege nawewe ukijua kila kitu, nakuamua kukaa kimya kama ujui vile. Unajiskiaje kuwa ambia watu wasiiamini ushirikina wakati nyie kwenye mikutano yenu mnahusudu mambo hayo(kumbuka ulipo omba kubadilishiwa kiti kwenye vikao vyenu vya nyuma. Na ukumbi wa Bunge kumwagiwa unga), unajiskiaje unaposema uwajui Richmond ingawa ukweli unawajua, unajiskiaje unapoamua kila hafla unapenda wewe kuwa mgeni rasmi, wakati nyingine nindogo sana ambazo hata makatibu wakuu wangetosha kabisa, nawenye hizi hafla wametambua udhaifu wako ndomaana kila upuuzi wanakuita. Nauliza unajiskiaje unapofanya biashara ikulu kwa mkono wanyuma(Riz 1), unajiskiaje kuamisha wanyama wetu na kuwapeleka Msoga naona umejenga zoo ndogo humo ndani. Unajiskiaje unaposema hela ya kuwalipa zaidi wafanya kazi hauna ila una wagharamia mawaziri kupita mikoani kutangaza mafanikio ya serikali yako, kama na wewe una yako ongezea humu.
 
Sina la kuongeza humu ndugu GNA.

Napita tu.

Lakini huoni unamsumbua Mh.Rais yuko mapumzikoni Serengeti?

Au kesharudi?
 
mh raisi unajisikiaje unapokuwa unapozunguka dunia ukitembeza kikapu huku ukiwa umekalia rasilimali nyingi,hivi huoni hizi gharama ugezitumia kwa mipango ya maendeleo kuliko kujidalilisha kwa kwenda kuombomba huku hauna uhakika wakupata
 
Duh hawezi kujibu maana ndo kwanza amealkwa kwenda kufunga saccos ya akina mama kule serengeti mapumzikoni
 
Jk unajisikiaje ukituambiaga uongo huku ukweli unaujua?
 
kwani mlitaka mimi nifanye nini kwaajili yao.??

Ninyi nyote mnao wazazi wenu, kwanini wasitafute pesa kuwapeni nyie...?

Ninayo miaka miwili tu ya kutawala,, subiri hao CDM wawape hizo huduma.

(without prejudice, am serious on what i've written above and that's what the President believeth in his heart).
 
2015 watawapa vitambaa,t shirt,kanga na vikoi,mbona mtawapa kura tu? Hamieni dijitali CDM tujikomboe mikononi mwa hawa mashetani
 
Back
Top Bottom