Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,673
Siku nzima ya leo nlikuwa kwenye tafakuri zito ya kinachoenda kutokea kwa nchi yangu baada ya wazungu kufanya yao.
Kwa sababu nliwahi kusoma uchumi kidogo. Naelewa kwamba kuna mipango mingi ya kimaendeleo itakumbwa na ukata na hata mingine ku kwama. Kwa sababu huu uchumi tulionao ni market economy and everything has a price tag. Kwa hiyo kwa maana nyingine bila kificho serikali inahitaji pesa.
Najua kuna mipango kutoka sasa itakuwa inasukwa ilikuangalia government revenue zinaongezeka vip. Lakini kwa hili tukio la ghafla hivi ni vigumu serikali iseme itakusanya kwa haraka fedha zote hizo mpaka wakati wa bajeti.
Ndo maana nikawaza kwamba huu ni wakati wa sisi wananchi kuipa serikali pesa. Ni wakati serikali iangalie uwezekano wa kukopa kwa wananchi.
Serikali itawezaje kukopa kwa wananchi? Ni kupitia kwenye halmashauri zake. Kuna kitu Amerika wanakiita municipal bonds.
Yaah serikali sasa inatakiwa kukopa pesa kwa ku issue municipal bonds kwa wananchi.
Mfano mrahisi wa jinsi itavokuwa. Mfano serikali imesema inapanga kujenga zahanati 10 katika mji wa mpwapwa dodoma. Inaweza kukadiria kwamba labda itahitaji kitu kama billion 1 kwa hiyo inachofanya itawapa kazi halmashauri ya mpwapwa wa issue municipal bond yenye maturity labda ya 5 years. Then inaweza kusema hiyo bond itakuwa na riba ya labda 10% kila mwaka. Sasa ikishakuwa hivo naamini raia wengi watajitokeza kununua bonds hizo kwa sababu hata na hivo hapa nchini kwetu kwenye ma benk mengi savings rate ni kati ya 4% kwa mwaka.
Sasa mfano tu kwa case ya mpwapwa ukapata watu kama 10000 wakanunua kwa wastani wa kila mmoja bond ya Tzs 100000 kila mmoja ina maana hapo umeshakusanya Tzs 1,000,000,000 ambayo haina magumashi halafu unajenga zahanati zako 10 halafu cha ku hakikisha ni kwamba kila mwaka halmashauri inatumia hizo zahanati kumi ili iweze kupata 100,000,000 za ku service hiyo municipal bonds.
Nadhani hii njia ni nzuri maana hata katika ujenzi wa hii miradi tunawatumia hao hao watanzania. Wakati pesa za misaada mpaka kandarasi zote ni makampuni yao. So pesa zinakuwa zinawarudia hao hao. Ila kama pesa zitatoka kwa wananchi na yakatumika makampuni ya wazawa kwenye jenzi hizi, pesa zitawarudia watanzania. Na huo ndo msingi na mwanzo wa kujitegemea.
Ko itakuwa jambo zuri kiasi. Kwa sababu hata serikali itakuwa inapata mikopo rahisi na uzuri zaidi wakopeshaji ni wananchi ambao pia ndio wanaonufaika moja kwa moja.
Nimesikia juzi serikali imekopa kama billion 100 japan lakini naamini kama ikitumika hii mbinu serikali inaweza kupata mikopo nafuu na rahisi isiyo na masharti na wakopeshaji ni sisi.
Ni hayo tu Rais wangu fanya tukakope kwa wananchi. Hata kama mtu ana 5000 tuzikusanye tu hizo hizo..
Tena huko vijijini hii ingekuwa safi sana maana unawapa watu alternative ya ku save pesa zao. Ukifika msimu wa kulima anaweza kuiuza hiyo bond akapata pesa yake akaingiza kwenye kilimo. Ni jambo moja zuri sana kwa kweli.