Tajiri la Bitcoin
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 1,139
- 707
Wanajamvi habari!
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni Bwana Ismail Maulid mkazi wa kijiji cha Mwanzi amethibitika kukamatwa na Ng`ombe wawili wa wizi wenye thamani ya Tsh Mil 3,600,000/= Chanzo cha ndani kinatanabaisha kuwa mwenyekiti huyu ni mwizi wa muda mrefu sasa, amekuwa akilindwa kwa ukaribu na viongozi wa Wilaya akiwemo mkuu wa Kituo cha Police Manyoni mijini.
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, Hata baada ya kukamatwa mwenyekiti huyo aliachiliwa baada ya masaa machache huku akiamuliwa kulipa ng`ombe hao ambao tayari alishawauza kwa mfanyabiashara mmoja wa Nyama katika Soko kuu la mjini Manyoni( Jina tunalihifadhi).
Mwenyekitu huyu ameonekana akijigamba hadharani kuwa yeye ndio serikali na hakuna wakumfanya chochote, Taarifa zinasema kuwa jambo hili limekuwa ni kawaida kwa baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Manyoni kiasi kwamba wanachi sasa wanaichukia sana serikali ya CCM.
Je adhabu ya kuiba ng`ombe nikulipa ng`ombe?
Je? Kwasasa kituo cha Polisi Manyoni kimegeuka Mahakama?
Wanajamvi ninaendelea kufuatilia na nitawajuza kila kitu kwa uwazi, kama kuna Polisi wamepewa Rushwa nitawaanika hapahapa kwa majina na kiasi walichopewa.