Rais wa Uturuki Erdogan: Nchi za magharibi zinapuuza sheria wakati damu za waislamu zinapomwagika

Mimi sio muislamu ila sifurahishwi na mauaji ya watu wasio na hatia yanayofanywa Kwa makusudi na Israel na Washirika wake Western Countries.

Naunga mkono hoja ya Erdogan
---
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameshambulia jibu la serikali za Magharibi kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza - akisema nchi za Magharibi hazichukui hatua kwa sababu "damu iliyomwagika ni damu ya Waislamu".

"Ni nini kilitokea kwa Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu?"Aliuliza."Wao [Magharibi] hawataitazama ikiwa haitoshelezi kusudi lao. Kwa nini? Kwa sababu damu inayomwagika ni damu ya Waislamu."

Jana, Erdogan alighairi safari ya Israel na kusema kuwa anajutia kusalimiana kwa mkono na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York mwezi uliopita.

Hayo yakiarifiwa waziri wa mambo ya nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina - ambayo inasimamia Ukingo wa Magharibi unaokaliwa lakini sio Gaza - alielezea mashambulizi ya anga ya Israel kama "vita vya kulipiza kisasi".

Akizungumza nchini Uholanzi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague, Riyad al-Maliki alisema shambulio hilo la bomu lilikuwa baya zaidi kuliko mashambulizi ya awali ya Israel, na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano.

Msemaji kutoka tawi la kijeshi la Hamas anasema takriban mateka 50 wanaoshikiliwa na wapiganaji wake huko Gaza wameuawa kutokana na Israel kushambulia kwa mabomu Ukanda huo, kufuatia mashambulizi ya kikatili ya Hamas tarehe 7 Oktoba.

Abu Ubeida hakutoa maelezo zaidi.BBC bila shaka haiwezi kuthibitisha idadi hii kwa njia huru

Jeshi la Israel limewatambua mateka 224 wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza.

BBC Swahili

View: https://twitter.com/ayubu_madenge/status/1718567131711742288?t=0nwGDa2DTa4VCFEdqsy8Eg&s=19
 
Back
Top Bottom