Rais wa Ufilipino kuvunja mkataba wa kijeshi na USA

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,830
20,257
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema Marekani inahatarisha usalama wa eneo kwa kuendelea kurundika silaha zake katika nchi hiyo.

Rais Duterte ameituhumu Washington kuwa inatengeneza vituo vya kudumu vya kuhifadhi silaha zake katika mikoa mitatu ya nchi hiyo.

Rais wa Ufilipino amesema: "Ninatoa ilani kwa vikosi vya jeshi la Marekani, sitoruhusu muendelee kuhifadhi silaha zenu katika ardhi yetu, hata hatufahamu kama makombora ya nyuklia yanaingizwa nchini na US au la."

Amebainisha kuwa, hatua hiyo ya Marekani ya kuingiza mashehena ya silaha nchini humo inakiuka moja kwa moja makubaliano ya ushirikiano wa kiulinzi kati ya nchi mbili hizo.

Ufilipino ilisaini makubaliano ya ulinzi na Marekani ambayo yamedumu kwa zaidi ya muongo mmoja sasa mbali na makubaliano mengine mapya yaliyosainiwa baina ya pande mbili mwaka 2014.

Oktoba mwaka jana, Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino alitangaza kuwa anataka ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo vikosi vya jeshi la Marekani viwe vimekwisha ondoka katika ardhi ya nchi yake; na kama italazimu anataka pia kuvunja mkataba wa ulinzi na muitifaki huyo wa muda mrefu wa Manila.

Wanajeshi wa Marekani nchini Ufilipino


Chanzo: IRIB
 
Avumilie tu kwa sasa serikali ya USA awamu hii ina kazi ya kufanya huyo Mfilipino asubiri kwanza.
 
Rodrigo Duterte,hana mamlaka ya kuvunja mikataba waliowekeana kati ya US na Ufilipino February 10, 1998, pia
Us nazobase Air base 5 ndani ya Philippines

1 Antonio Baustista Air base
2 Basa Air base
3 Fort mogsaysay Air base
4 Lumbia Air base
5 Mactano- Benito ebuen Air base
Pia ndani ya US fillipino ndio jamii namba tatu kwa ukubwa kwa jamii ya wahamiaji ndani ya USA huku idadi ya wahamiaji ndani ya US wakiwa 41.3 milion huku filipino wakiwa ni 3,416,840 na kuifanya ni jamii ya tatu kwa ukubwa ya wahamiaji hawa tayali wana uraia wa US hii ni kwa mujibu wa US department of homeland security
So mahusiano ya US na phillppines ni mazuri ila yalikuja ingia sintofahamu baada ya rais
Rodrigo Duterte mpaka kufikia kumtukana rais wa US mr Obama "sun of *******" na kufikia hatua ya kutaka kuzifunga kambi zote za US nchini kwake lakini ilo alitawezekana kiwepesi kama anavyosema yeye kwani walisaini mikataba pia wazungu wanaposaini mikataba na watu wengine nje ya jamii yao huwa wanaweka vipengere ambavyo ni vigumu kuvunja na kama utavunja unaweza kujikuta umeingia kwenye gharama kubwa sana au mgogoro utakaopelekea kuwekewa vikwazo.

Sasa kinachosumbua ni kuwa siasa za dunia zmebadilika kutoka siasa za kibepari mpaka siasa za utengano kila nchi kufunga mlango na bahati mbaya anayetaka siasa hzo ni mtu mwenye nguvu na ushawishi duniani Mr D. J Trump na hapa namnukuu

" For many decades , we' ve enriched foreign industry at the expense of American industry subsidized the armies of other countries , while allowing for the very sad depletion of our military . We ' ve defended other nations' borders while refusing to defend our own .
And spent trillions and trillions of dollars overseas while America ' s infrastructure has fallen into disrepair and decay "
Sasa kinachofata ni kuchangia cost kwa majeshi ya US kulinda nchi au mipaka yako sasa Japan,south korea na phillppines na kuna uwezekano mkubwa kwa US kufunga baadhi ya base zake 800 military bases in more than 70 countries and territories abroad, nje ya hapo hawezi kufanya lolote kuhusu majeshi ya US ndani ya Ufiiipino
 
Back
Top Bottom