Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,230
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini Tanzania TAHLISO Bw. Geofrey Kiliba amesisitiza umuhimu wa Wasomi na Vijana waliopo vyuoni kukemea, kukosoa na kushauri kwa kutumia maarifa na taaluma zao katika kuijenga Tanzania na kuepusha waharibifu wanaotishia kuharibu misingi ya amani, utulivu na mshikamano ulipo nchini Tanzania.
Kiliba amebainisha hayo leo Agosti 02, 2025 wakati akiongoza Kikao cha Seneti cha Jumuiya hiyo, Kikao kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam akibainisha kuwa jambo pekee na la muhimu linalotoa fursa kwa wasomi kuzungumza na kukosoa ni maarifa waliyonayo katika kuijenga Tanzania njema na yenye kutoa fursa ya kila mmoja kustawi kupitia misingi ya utu, amani, utulivu na uhuru wa kutoa maoni.