Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Rais Magufuli na Rais Shein walipokuwa wakiapishwa katika nafasi zao, wote wawili waliapa kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunaamini hiki ni kiapo serious kabisa, si jambo la mzaha.
Kumekuwa na matukio kadhaa ambayo imeonekana kama Rais Magufuli amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati fulani huko Zanzibar suala la Mswaada wa Mafuta na Gesi huko Zanzibar lilionekana kwamba ni uvunjaji wa makusudi wa Katiba ya Tanzania iwapo Rais Shein angetia sahihi - Na bila kusita Rais Sheini aliutia ule muswaada sahihi hata akiungwa mkono na waziri wa Nishati Tanzania ambaye ni waziri wa Muungano. Kwa upande wa Muungano, suala la kuteua wabunge sita wa kiume lilionekana pia ni uvunjwaji wa Katiba kwa upande wa Rais Magufuli.
Sasa ili tusije tukajenga utamaduni kwamba Rais wa Tanzania au Zanzibar wanaweza kwa makusudi tu au bila kukusudia wakavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasifanywe lolote, inapaswa iwekwe wazi kabisa kwa wananchi wote, utaratibu au hatua za kisheria ambazo zinapaswa kuchukuliwa na hata yule mwananchi wa kawaida kabisa kule kijijini, iwapo itaonekana Raisi wa Tanzania au Zanzibar amevunja Katiba ambayo aliapa kuilinda.
Ni jinsi gani mwananchi wa kawaida wa Tanzania amewezeshwa kumchukulia hatua Rais wa Tanzania au Zanzibar pale inapoonekana kwa makusudi au bila kukusudia amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoapa kuilinda?
Kumbuka kuvunja Katiba sio suala la kusema hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Rais itapelekwa Bungeni au Baraza la Wawakilishi; hapana, mwanzo wake unatakiwa uwe ni uthibitisho wa kisheria kwamba kweli Katiba imevunjwa, na kisha hatua ya kuwajibishwa ifuatie.