rais wa awamu ya nne na hotuba ndefu kwa wazee wa jiji la Dar.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Rais wa awamu ya nne alikuwa na tabia ya kuwahutubia wazee wa jiji la Dar, hata kama anayoyaongelea hayawahusu. Na mara nyingi mtu mwenye umri mkubwa kuanzia miaka 70, huwa hawezi kuzisikiliza hotuba ndefu za wanasiasa. Atajitahidi kusikiliza kwa dakika ishirini, baada ya hapo anaanza kusinzia. Kama wapo wazee mia mbili wanaosikiliza hotuba ya Rais, basi wanaoweza kusikiliza mpaka mwisho wa hotuba bila ya kusinzia hawafiki hamsini.

Sidhani kama nitakuja kusikia eti rais wa awamu ya tano anawahutubia wazee wa jiji la Dar, halafu ujumbe wa hotuba yake wala hauwahusu wale walioketi wakimsikiliza. Ule utaratibu wa kuhutubia wazee ni muendelezo ule ule wa majungu na maisha ya mtu anayetaka kuonekana mwema kwa kila mtu. Nategemea kuuona uongozi wa kisayansi, unaotatua matatizo kisayansi bila ya uswahili mwingi.
 
Waliokuwa wakiitwa wazee hawakuwa wazee kwa maana ya umri peke yake bali nafasi zao katika jamii. Mfano walikuwa wenyeviti wa mitaa, maafisa watendaji wa mitaa na kata na makatibu wa CCM. mantiki ya kuongea na wazee haikuwepo kwani hapakuwa na mabadilishano ya hoja bali hotuba ndefu ya rais kama ulivyosema.
 
Back
Top Bottom