Rais ukitaka kuboresha sekta ya maji wapatie mafunzo watanzania

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Jana nimesikia kwenye vyombo vya habari kuhusu Raisi kutoridhishwa na utendaji wa miradi ya maji.

Ki msingi mweshimiwa raisi changamoto kubwa katika sekita ya maji ni "nchi kutokuwa na wataalamu wenye weledi katika kutatua changamoto za maji"

inasemekana huko nyuma wizara iliyohusika na maji ilikuwa ikiendesha ujenzi wa miradi ya maji kwa wizara yenyewe kuwa "client", mshauri na mkandarasi. Pande zote tatu walizishikilia wao wenyewe.

lakini ilifika wakati wakashauriwa kuwa ili kuleta tija katika miradi ya maji ni vema wizara ibaki kama mmiriki wa mradi yaani "client" na kwa upande wa ushauri yaani consultancy basi awepo mshauri mwenye uzoefu wa kazi zinazofanyika za mradi ili amshauri mwenye mradi mambo ya kifedha, kisheria na kiufundi. lakini pia atafutwe mwingine ambaye ana uzoefu na ujuzi wa kutekeleza miradi ya aina hiyo ili atekekeleze miradi hii kwa niaba ya mwenye mradi.

Lengo la kuingiza pande tatu za utekelezaji wa miradi ilikuwa ni kuongeza weredi ili kuleta matunda makubwa zaidi katika utekelezaji wa miradi.

Kama ulivyosema raisi kuwa fedha za miradi ya maji zinazotolewa haziendani na matunda yanayotoka katika miradi hiyo basi hii inaonyesha kuna changamoto zilizojitokeza katika jambo hili ambazo zinaturisha hatua kama ile tulipofanyia maamuzi ya kusema wizara ibaki mmiriki tu na kazi ya kusimamia mambo ya kiufundi ya miradi na fedha yafanywe na wazabuni binafsi na kazi ya ujenzi ifanywe na wazabuni binafsi.

Ki msingi hatua hii ilikuwa ni muhimu sana na ndiyo njia ya kuboresha utekelezaji wa miradi ila kwa sasa njia hii inahitaji kutazama changamoto zinazoikabili.

Changamoto za sasa.
1. Utekelezaji wa miradi hunafanywa na Sekita binafsi huku serikali ikibaki kama mmiriki. Sekita binafsi hawa wanapoachwa bila kutungiwa kanuni za ni jinsi gani wafanye kazi basi wao hujikita katika kujilimbikizia faida kwa kujaribu kutumia gharama kidogo sana kutekeleza mradi ili faida mwisho wa mradi iwe kubwa.

ili mradi wa maji ufanyike kwa ufanisi unahitaji kuwa na wataalamu wa fani nyingi, unahitaji wahandisi wa ujenzi "civil and water resources engineers", unahitaji wahandisi wa mitambo kwa maana ya pampu na mitambo mingine "mechanical engineers", unahitaji wahandisi wa umeme", unahitaji land surveyors, unahitaji quantity surveyors, unahitaji wataalamu wa kutengeneza michoro "AUTOCAD Technicians", unahitaji wahasibu au wataalamu wa fedha ili kuratibu matumizi ya fedha, unahitaji madereva wa magari ya miradi, unahitaji ma "secretaries" kwenye maofisi, unahitaji wataalamu wa udongo, unahitaji wataalamu wa miamba, unahitaji wa shughuli za ujenzi.

Ki msingi changamoto kubwa ni serikali kudhani kazi ya mmiriki ni kutafuta fedha za kutekelezaq miradi na kusikiliza miradi imefikia hatua gani na kuidhinisha fedha za kuwalipa makandarasi au washauri basi. Sekita hii imebaki haina msimamizi wa kuangalia jinsi gani tunatengeneza jamii yetu kuwa endelevu katika miradi hii.

kutokana na kukosekana usimamizi huu wa serikali kusimamia kanuni za mchezo wa utekelezaji wa miradi, afanya biashara hawa ambao wanafanya ukandarasi na ushauri wametumbukia katika ubabaishaji wa hali ya juu.

1. wazabuni hawa wanatumia Curriculum vitae nzuri lakini wakipata kazi wanatumia watu wa ovyo ili mradi wamaximize profit, Je ni nani ana wajibu wa kutizama hili je ni wizara, ni mshauri wao yaani "consultant"? Ma consultant wenyewe wanafanya haya, Je ndani ya wizara wanatizama haya?

2. wazabuni hawa wanaajiri kwenye miradi wataalamu wchache sana mathalani kampuni ya ushauri wa mradi inaajiri wahandisi wawili, Civil engineers tu na kuwapa secretary mmoja, hawa ndio wanaosimamia mambo yote, kama mambo yanahusu utaalamu wa miamba, wanashauri wao wakati miamba sio taaluma yao, kama ni mambo ya Land survey wanafanya wao, kama ni mambo ya Quantity survey wanafanya wao, kama ni kusimamia ujenzi wa majengo ni wao, kama ni kusimamia ulazaji wa mabomba ni wao, kama ni mambo ya mitambo ni wao wakati si taaluma yao, kama ni mambo ya umeme ni wao wakati sio taaluma yao, watu hawa hawana madereva magari wanandesha wao wenyewe, watu hawa ndio hufanya shughuli za kihasibu katika maofisi yao.

Huu ni ubabaishaji wa hali ya juu. Haiwezekani tutumie mabilioni ya fedha kutekeleza miradi alafu turuhusu ubabaishaji wa hali ya juu katika kutekeleza miradi hii, wafanya biashara wanatuwekea vivuli kwenye miradi, hakuna anayejali alafu mwisho wa siku tunajiuliza kwa nini? Nani anawajibika kusimamia haya?

Ni gharama ndogo sana kuweka mtaalamu katika mradi kuliko kuondoa wataalamu tukapoteza fedha zetu tunazoziweka kwenye miradi.

Nini kifanyike

Wizara au serikali itunge kanuni za musimamia utekelezaji wa miradi.
1. kwa yeyote anayetekeleza mradi kwa kulipwa fedha na serikali iwe wakandarasi wajenzi au wakandarasi washauri ni sharti taaluma zote zitakazoainishwa na wizara kuwa zinahusika katika utekelezaji wa mradi ziwepo katika eneo la mradi wakati shughuli husika zinafanyika kuanzia mwanzo wa shughuli mpaka kukamilika kwa shughuli. kama ni ujenzi wa jengo basi lazima mchora ramani ahusike, lazima structural engineer ahusike, lazima mtu wa mifumo ya maji awepo, lazima mtu wa umeme awepo ilimradi pale tu shughuli zake zinapofanyika.

2. Ni lazima tutengeneze jamii inayorithishana utaalamu hivyo katika miradi ni lazima kwa taalauma zote kuwepo experienced "seniors" and juniors ambao wanatafuta maarifa. Ni makosa makubwa yanayofanyika sasa mfano consulting firms zimekuwa zikitafuta retired experts kutoka nje ya nchi na wanapokuja hapa wanafanya kazi bila ku "engage locals" Mfano kuna kampuni moja inasimamia miradi ya maji Lindi, Sumbawanga, Kigoma, Musoma, nk, kama wakandarasi washauri, katika miradi hii yote wana An old man "retired" kutoka nje ndiye anazunguka katika miradi hii huku anakaa wiki moja ana hamia kule anakaa wiki moja nako anahamia kule.

Kila mwaka vyuo vyetu vinatoa wataalamu wanaohitimu katika vyuo vyetu katika fani za mechanical na umeme, kila mwaka tunahesabu tunaongeza wingi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hivyo ku project ku create ajira nyingi zaidi, ni kwa nini hatutizami kanuni ili kuwalazimisha watu wetu kuajiriwa katika miradi hii hata ikiwezekana wafanye kazi chini ya uangalizi wa hawa expatriate kutoka nje ili wawaachie maarifa waliyokuja nayo.

3. Ni lazima tutengeneze Local experties katika kutekeleza miradi. Hii ina faida kiuchumi na kitaaluma. Wahindi wakitukopesha fedha basi wakandarasi na washauri katika fedha hizo tunachukua kwao mfano mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu juu pale mlandizi, fedha ilitoka india hivyo mkandarasi india na mshauri india. Mradi wa kutoa maji Shinyanga kwenda Tabora Fedha tumekopeshwa kutoka india, mkandarasi katoka india na mshauri india. Hatuwezi kuwalaumu kama hayo ndiyo masharti yao ya kukopesha fedha hivyo tuna hiari ya kuchukua fedha zao na kuwatumia au kuviacha vyote. Tujilaumu wenyewe kwa kutokuwekea fedha zetu masharti ili fedha hizo zitekeleze miradi kupitia watu wetu hivyo kurudi kwenye mzunguko wetu na pili fedha hizo zitumike kujenga ujuzi zaidi kwa watu wetu.

Tusitegemee vyuo vyetu kutoa ma expert katika taaluma kwani elimu za vyuoni ni kwa ufupi sana "general knowledge", ma expertise hutengenezwa na experience. Tusiogope watu wetu kushindwa cha msingi tuweke vigezo vya kubaini watu sahihi na kuwapa exposure ya kuwasukuma kutekeleza miradi. tukijenga tabia hii, ndani ya miaka 10 tutajitosheleza na kupunguza sana utegemezi wa nje na tukifika hapo gharama za utekelezaji miradi zitashuka sana lakini pia tutaokoa pesa nyingi zinazochukuliwa na makampuni ya kigeni na fedha hizo kuzitumia kununua bidhaa nyingine zenye umuhimu kutoka nje. Lakini pia tujilaumu kwa kutokuweka masharti ya makampuni ya nje kuja kufanya kazi kwetu. India wanapotupa fedha ndiyo hiyo fedha ni yao lakini lazima tutambue huo ni mkopo sio msaada, kama ni mkopo tunaweza kutafuta jinsi ya kufaidi fedha hizo zaidi mfano kwa kuweka sharti la kila kampuni ya nje ikija kufanya kazi kwetu ni lazima itafute 40% local joint venture ndio ikubalike kisheria kufanya kazi nchini.

bila kutengeneza local experties ambao wamejengewa uwezo wa kupima vyanzo vya maji na kuyabaini haijalishi maji yanayonekana au hayaonekani tukabaki kulea ubabaishaji wa wafanyabiashara kutumia wataalamu wasio wenyewe kubaini vyanzo vya maji tutabaki kulipa atu kufanya upembuzi yakinifu, kulipa washauri na wakandarasi lakini tukichimba visima havitoi maji.

bila kutengeneza local experties nyingi ya kutosha tutabaki kuwa na wahandisi wachache wakisimamia ulazaji wa mabomba huku hawapati mda wa kupumzika au kutafakari na tunaposukuma maji mabomba yanapasuka. Umemuweka mtu kusimamia kwa niaba yako, anapitisha na kuidhinisha fedha ulipe na matatizo yanapotokea kwa nini usimkamate huyu aliyekuwa akisimamia kwanza kuwa alikuwa wapi?

bila kutengeneza local experties ya kutosha ya wataalamu wa umeme katika maji tutabaki tunajiuliza kuwa ni kwa nini hatufanyi miradi ya solar kwenye maji na tunaendelea na magenereta yenye running cost kubwa, tutabaki kwenda vijijini tukiwawekea mifumo ya automation kama scada yenye running cost kubwa wakati mamlaka zenyewe haziwezi kujiendesha sawa na kumshauri mwenye genge kutumia kompyuta eti inarahisha mahesabu.

bila kutengeneza locals wataalamu wa pump za maji ambao ni mechanical engineers wafanye shughuli za pump kwenye miradi ya maji tutabaki na wababishaji wakifanya maamuzi ya vitu wasivyovijua na mwisho wa siku ni kuzipatia mamlaka mitambo inayotumia gharama kubwa kukarabati, mitambo inayokula umeme mwingi kusukuma maji kidogo na tutabaki kulalamika mamlaka kushindwa kujiendesha.
 
Kwani ameanza lini kupokea ushauri?

Hakuna binadamu asiyepokea ushauri ila kila mmoja ana namna yake ya kushauriwa hivyo tusikimbilie kusema raisi hashauriki bali sema unachoona kinafaa na yeye atachambua kama ataona kinaingia kwenye ilani yake atakichukua anavyojua na akiona hakiingii atakiacha.

anayeshauriwa ana hiari ya kuchukua au kuacha ushauri
 
Hakuna binadamu asiyepokea ushauri ila kila mmoja ana namna yake ya kushauriwa hivyo tusikimbilie kusema raisi hashauriki bali sema unachoona kinafaa na yeye atachambua kama ataona kinaingia kwenye ilani yake atakichukua anavyojua na akiona hakiingii atakiacha.

anayeshauriwa ana hiari ya kuchukua au kuacha ushauri
Nikukumbushe tu Siku anazindua mabasi ya mwendo kiasi alisema "Niligombea mwenyewe wala hakuna mtu aliyenisindikiza kuchukua fomu"
Tafuta hiyo clip kama hujawahi iona
 
Back
Top Bottom