Mhe. Rais kwa heshima na taadhima tunakuomba utusaidie kwa uwezo ulio nao kutukomboa kwenye adha kubwa tunayopata wananchi wako waishiyo kando kando ya barabara inayotoka Buswelu mpaka barabara ya lami ya Mwanza -Musoma. Mhe. Rais suala hili tumemueleza Mhe. Mbunge wetu wa Ilemela bila mafanikio. Mhe.Rais baadhi ya adha tunaayokumbana nayo ni kama yafuatayo:-
Mhe. Rais tunaomba utusaidie. Tumemueleza Mhe. Mbunge wetu wa Ilemela bila mafanikio.
- Kwa siku inakadiriwa kuwa takriban magari 1500 yanapita kwenye njia hiyo na vumbi inayotifuliwa na magari hayo inatisha.
- Uchafu unaotokana na vumbi hiyo kwenye vyakula vyetu, matandiko yetu na nyumba zetu inatisha.
- Watoto wetu wanapata kikohozi kisichoisha kwa sababu ya vumbi.
- Wafanyabiashara kando kando ya barabara hiyo wamekimbiwa na wateja na wengi wamefunga biashara zao na hivyo kukosesha Serikali mapato.
- Watoto wa shule kando kando ya barabara hiyo mfano Gedeli, Eden Valley wakohatarini kugongwa na magari kutokana na vumbi inayotifuliwa.
Mhe. Rais tunaomba utusaidie. Tumemueleza Mhe. Mbunge wetu wa Ilemela bila mafanikio.